Kiongozi wa mila tarafa ya Ngorongoro, Augustino Pakai Olonyokei akizungumza na Meneja uendeshaji wa mtandao wa habari wa Zainul Mzige aliyefika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia miradi
mbalimbali inayoendeshwa kusaidia jamii ya wafugaji wa kimasai hivi
karibuni.
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
KIONGOZI
wa mila tarafa ya Ngorongoro Augustino Pakai Olonyokei ameitaka
serikali kusimamisha uwekezaji katika Mamlaka ya Ngorongoro ili
kupunguza shinikizo la raslimali katika eneo hilo.
Alisema
kuendelea kuwekeza katika mahoteli,makambi ya watalii, miundombinu
katika hali ilivyo sasa ni kuzidisha migogoro iliyopo kati ya wakazi wa
eneo hilo na mamlaka ambayo tayari ipo.
Olonyokei
alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na mwandishi wa habari
hizi ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia miradi mbalimbali
inayoendeshwa kusaidia jamii ya wafugaji wa kimasai.
Alisema
hali ya sasa ni ngumu na inayosikitisha hasa kutokana na sheria
iliyoanzisha mamlaka ya Ngorongoro kuwanyang’anya umiliki wa eneo ambalo
wao wamelilinda miaka yote ndiyo maana wanyama wanapatikana na utalii
unakuwepo.
Aidha
alisema mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya mazingira yao kuwa magumu ,
wanakuwa na njaa huku wakiwa wamekatazwa kulima hata eneo dogo.
“Tuna
changamoto nyingi…hatuna ajira, ushiriki wetu katika bodi ni mdogo na
baraza la wafugaji linapewa hela kidogo katika mazingira ya kuwa na
miradi mingi,” alisema Olonyokei.
Alisema Baraza hilo kupewa sh bilioni moja tu haitoshi wakati utalii ukiingiza mabilioni ya fedha.
Pamoja
na kuelezea changamoto hizo na kuitaka serikali kuzuia kuongezeka kwa
shughuli zaidi katika eneo hilo, aliwataka watanzania kujua mazingira ya
jamii ya wafugaji na adha wanazokutana nazo.
Hata
hivyo Mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro Dk. Freddy Manongi amesema
kwamba pamoja na malalamiko hayo, mamlaka hiyo iliyoanzishwa mwaka 1959
kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii, utalii na kuhifadhi mazingira
mwaka jana pekee ilitumia sh bilioni 60.
Fedha hizo ni kwa ajili ya kuhifadhi, kuendeleza jamii na utalii.
Alisema
msaada mkubwa wanaoufanya ni katika sekta ya elimu ambapo imejenga
shule 21 na kila mwanafunzi anayekwenda sekondari kutoka katika eneo
hilo hupatiwa udhamini wa masomo.
Aidha
alisema kutokana na wananchi kuzuiwa kulima, huwapatia mahindi kwa
ajili ya chakula na ingawa kunatakiwa kuangaliwa namna bora zaidi
endelevu ya wananchi kupata chakula lakini kwa sasa hilo ndilo
wanalofanya.
Mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro, Dk. Freddy Manongi katika mahojiano maalum na Meneja uendeshaji wa mtandao wa habari wa. Zainul Mzige (hayupo pichani).
“Mahindi ya bure yanapokosekana anagalau yawepo ya kununua kwa bei ya chini, na tunauza kwa shilingi 5000 kwa debe” alisema.
Dk.
Manongi alisema pia kwamba fedha nyingine zinatumika katika sekta ya
afya na pia kuboresha hali ya mifugo kwa kuwezesha uharamishaji mifugo
na kujenga majosho.
Alisema
ongezeko kubwa la watu katika eneo ambalo haliongezeki ni dhahiri
linaleta migongano lakini mamlaka hiyo inafanya shughuli zake kwa
kushirikiana na Baraza la wafugaji ili kupunguza migongano.
Wakati
mamlaka inaanzishwa 1959 eneo hilo lilikuwa na wakazi 8,000 baada ya
wengine 4000 kuhamishiwa hapo kutoka Serengeti. Kwa sasa eneo hilo lina
watu takaribani 90,000 katika eneo lilelile la kilomita za mraba 8,262.
Alisema
baraza hupewa sh bilioni 2 kwa mwaka wakati shughuli nyingine za
maendeleo zinazofanywa na Mamlaka hugharimu sh bilioni 11.
Kuhusu
changamoto za elimu amesema kwa mwaka jana hali haikuwa njema kwa
ufaulu lakini sasa wametafuta sababu na kuanza kuhakikisha kwamba walimu
wanapewa motisha na pia wanafunzi wanapata mlo wa mchana ili kuwafanya
wasitoroke.
Kuhusu
suala la ajira Dk. Manongi amesema ni tatizo la tafsiri tu lakini kila
nafasi zinazpopatikana hujitahidi kuajiri watu kutoka katika eneo hilo.
Alisema
kuna mambo mengi yanayofanywa kuimarisha eneo hilo kuendeleza jamii na
kuendeleza hifadhi ili kuwezesha utalii ambao ndio unatoa fedha kwa
ajili ya mambo yote.
0 comments:
Post a Comment