2015-03-18

Ajali ya basi la FM Safari na Fuso imeua wawili na kujeruhi watatu Mikumi Morogoro.


Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujerihiwa baada ya basi la FM safari likitokea Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya kugongana uso kwa uso na fuso iliyo sheheni nyanya katika eneo la hifadhi ya mikumi barabara ya Morogoro Iringa. 


Wakizungumza na ITV mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lingine na hivyo kugongana usokwa uso ambapo wametupia lawama baadhi ya abiria kuwachochea madereva kuendesha kasi na ambapo wameshauri vyombo vya usalama barabarani kuwachukulia hatua madereva wazembe wanaosababisha vifo visivyo vya lazima. 


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amewataja walio fariki katika tukio hilo kuwa ni Seth Mapunda ambaye ni dereva wa fuso na mwanamke mmoja ambaye hajafahamika majina yake na jeshi la polisi linamshikilia dereva wa basi kwa kusababisha ajali. 

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...