Kwa mujibu wa gazeti la Visa, limeripoti kuwa kuna fununu kuwa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja anadaiwa kurudiana na mzazi mwenzake P Funk Majani ambaye ni mtayarishaji nguli wa muziki wa Bongo Fleva.Hii ni kutokana ka bwana’ke amabe alimpora Wema Sepetu , CK kudaiwa kuishiwa mkwanja.
Licha ya kuwa Kajala bado yupo kwenye ndoa na mumewe anaesota gerezani, inadaiwa kwasasa anajipooza machungu na kushea mashuka ya hoteli na mzazi mwenzie P Funk.
kwa mijibu wa gazeti hilo marafiki wa karibu wa Kajala waliliambia kuwa mara kadhaa Kajala amekuwa akitoka na P Funk kwa kificho, kwa kile kilichodaiwa anamwogopa mwandani wa sasa wa Majani.
Gazeti hilo liliendelea kueleza kuwa Kajala kwa sasa yupo dabo kwenye mahusiano na CK , bwana wa zamani wa Wema ambaye kwasasa hali yake ya kiuchumi haina tofauti na Mr Nice.
Inadaiwa kuwa kinachosababisha ukaribu kati ya Kajala na P Funk ni mtoto wao Paula ambae kwasasa wanashirikiana vya kutosha kumlea.
0 comments:
Post a Comment