2015-03-23

HATARI! BINTI MIAKA 14 ASUTWA KWA UTAPELI


    Latifa anayedaiwa kwa utapeli.

Binti wa miaka (14) aliyefahamika kwa jina la Latifa amejikuta akisutwa kwa utapeli baada ya kunaswa na OFM akijifanya ni mtoto asiye na wazazi wala ndugu wa kumsaidia.Binti huyo aliwasimulia waandishi wetu kuwa baba yake alimtelekeza kwa majirani huko Dodoma maeneo ya Kibaigwa kwa kile alichodai kuwa baba yake alikuwa na madeni yaliyosababisha mali zake kupigwa mnada na yeye kusakwa ndiyo maana alikimbia. 
        
Latifa alisimulia kuwa kwa kuwa hakuwa na ndugu yeyote aliyekuwa akimfahamu alilazimika kuishi maisha magumu ya kuhamahama akiwa peke yake ambapo alidai alikimbilia kwa ndugu wa baba zake mkoani Lindi ambapo huko alikutana na kasumba ya ukeketaji na kukimbilia jijini Dar. 

Akiwa Dar Latifa aliwasimulia waandishi wetu kuwa alikuwa akifanyishwa kazi nyingi kama hausigeli ndani ya nyumba moja maeneo ya Tegeta ambapo pamoja na hayo alikuwa akinyanyaswa sana. 

Alizidi kudai kuwa aliamua kukimbilia Kijitonyama akiwa kama mzururaji ambapo alikutana na madada wanaojiuza ambao alidai kuwa walimchukua na kuishi naye mpaka alipokutana na waandishi wetu ambao aliwaomba msaada kwa madai hakuwa na chakula wala mahali pakulala . 


 
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael.
 
AANZA KUSHTUKIWA
 
Hata hivyo, baada ya kupelekwa kwa mfadhili aliyeahidi kumpa malazi binti huyo, alimshangaza mwenyeji wake kwa kupigiwa simu mara kwa mara na watu ambao hakuwaweka wazi. 
Alipopekuliwa kwenye simu ndipo namba za watu waliogundulika kuwa ni ndugu zake walionekana na walipopigiwa walikiri kumfahamu Latifa kama ndugu yao na kuanika siri kwa nyakati tofauti kuwa kweli Latifa hana mama lakini tabia za utapeli zimemfanya afukuzwe kwa kila ndugu anayeishi naye. 

“Yaani huyo mtoto hakuna mtu anayetaka kuishi naye mimi mwenyewe ameshaniliza na simtaki aje kwangu, nyie cha msingi mtoeni hapo nyumbani kwenu yasije yakawakuta,” alisema kaka yake aliyejitambulisha kwa jina la Saidi kauli iliyotiliwa mkazo na mama yake mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Mwazani. 


                             Jacqueline Wolper.
 
Hata hivyo, waandishi wetu waligundua kuwa msichana huyo kwa nyakati tofauti alienda nyumbani kwa wasanii wa filamu, Wema Sepetu, Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael kwa nia ya kutaka wamasaidie lakini kashitukiwa na kutimuliwa. 

“Nilienda kwa Wema nikagonga akatokea msichana akaniambia Wema hayupo nikawa narudia mara nyingi lakini mwishoni akanifokea.
 “Nikaenda kwa Lulu lakini mama yake alinifukuza na kwa Wolper niliambiwa alipokuwa akiishi alishahama,” alisema msichana huyo aliyedai yote aliyofanya ni kutokana na ugumu wa maisha hivyo asitiriwe.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...