Staa na mrembo kutoka Bongo Movies, Irene Uwoya, amewataka wasanii chipukizi wenye ndoto ya kuigiza naye katika filamu yake mpya wawasiliane naye ili awajumuishe katika filamu hiyo.
Uwoya alitoa fursa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alisema, anafanya hivyo ili kunyanyua wasanii chipukizi wanaokosa nafasi za kuigiza na mastaa licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa uigizaji.
“Najiandaa kwa ajili ya kazi yangu mpya na natumaini itakuwa nzuri kwani hatua niliyofikia ni kutoa nafasi kwa chipukizi kushiriki filamu hiyo kwa kuwa ni jambo la busara,” alieleza Irene.
Irene ambaye amejijengea umaarufu mkubwa kupitia filamu yake ya ‘Oprah’, aliyoigiza na Kanumba ambaye ni marehemu kwa sasa, ametamba kuendelea kuibua vipaji vipya zaidi vya wasanii wa filamu.
0 comments:
Post a Comment