Umwagaji wa Cement ukiendelea
Picha ya Jana Kabla ya Kumwaga Cement Katika Barabara ya Mwanga Rusimbi
Wakipima kwa ajili ya kumwaga Cement
Vibaluwa wakiendeleza kazi yao
Daraja likiwa katika hatua za ujenzi makutano ya Barabara ya Rusimbi na Kisangani ukiwa unaelekea Mlole na nyumba inayo onekana hapa ni Jengo la Msikiti uliopo Mtaa wa Kisangani
Gari lililobeba Cement likiwa tayari kwa ajili ya kushusha Cement
Katika kuhakikisha mkoa wa Kigoma unapiga hatua kimaendeleo kumekuwa na mradi wa ujenzi wa barabara za mitaani unaoendelea hivi sasa,miongoni mwa barabara zinazojengwa katika kiwango cha lami na kampuni ya wachina ni hii ya Lusimbi inayotokea mtaa wa Shaurimoyo Mwanga kupitia barabara kuu ya Lumumba,Legezamwendo,Mabatini na inakuja kutokea Pefa Ujenzi jirani kabisa na Kanisa la Efatha Ministry ambayo inakutana na Kasulu Road,zingine barabara zinazojengwa ni ile ya M/mwema ikianzia maeneo ya Bima Kigoma Mjini kupitia Website kwenda mpaka Bangwe jirani na Power Station ya Tanesco na nyingine ni ile ya Gungu kupitia Mwasenga Eria kuja kutokea Katubuka Manguruweni,mpka sasa karibu barabara zote hizi zipo katika hatua za mwishoni kabisaa kumalizika kwani kama uonavyo katika picha hapo barabara zote zimeshawekwa Cement na hii ndio iko inamaliziwa kuwekwa.
kwa taarifa kama hizi za nyumbani Kigoma endelea kutembelea mtandao wetu huu wa kigoma24hours.blogspot.com kila mara na unaweza kulike ukurasa wetu wa facebook (Page) ili tuwe tunakusogezea kila habari inayotufikia toka nyumbani Kigoma,bonyeza hapa ujiunge nasi moja kwa moja facebook,bofya==>''HAPA''
0 comments:
Post a Comment