Marais
wa nchi sita za Afrika watakuwa na mkutano mkubwa leo Jijini Dar es
Salaam ncini Tanzania ambapo watajadili kwa kina juu ya kuboresha
uwekezaji katika kanda ya Maziwa Makuu. Marais hao ni Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Pierre
Nkurunziza wa Burundi, Paul
Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na
mwenyeji wao wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano huo wa siku mbili utaambatana na mdahalo baina ya viongozi
hao na wadau mbalimbali katika sekta za biashara na
maendeleo. Mjadala
wa viongozi hao utajikita katika umuhimu wa Ukanda wa Kati ambao ni
kiungo muhimu katika ukuaji uchumi wa nchi hizo kwa kuwa husaidia katika
uingizaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali kupitia Tanzania kwa njia za
maji, reli na barabara. Wakati wa mkutano huo, viongozi hao watafanya
uzinduzi wa treni ya mizigo kuelekea Uganda, Rwanda na DRC.
0 comments:
Post a Comment