2015-03-04

MASTAA WAMCHARUKIA TIBAIJUKA NA KUDAI KWA HIKI ALICHO KIFANYA ANASTAHILI AZABU


KAULI ya aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kuwa kiasi cha shilingi milioni 10 alizotoa haraka kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow alizowekewa na 
mfanyabiashara James Rugemalila zilikuwa ni za mboga, zimewakera mastaa kiasi cha kumshambulia na kumuita mwenye dharau iliyopitiliza.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Tamlina Posh 'Amanda'.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar kwa njia ya simu, walisema fedha hizo ni nyingi ambazo zingeweza kuwasaidia wagonjwa mbalimbali, uchimbaji wa visima, kusaidia elimu, chakula kwa familia 
zisizojiweza na makundi mengi yenye uhitaji. Walisema kauli hiyo inaonyesha jeuri waliyonayo watumishi wa umma, ambao hupata fedha nyingi kwa njia zisizo halali kiasi cha kufikia hatua ya kukufuru. Mastaa hao ni pamoja na Baby Madaha, Nisha, Thea, Isabela, Tiko na Amanda Poshi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...