KUFUATIA sintofahamu kati ya wapenzi wawili, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Siwema Edson juu ya mtoto wao mwenye umri wa miezi mitatu, mwanaume huyo amesema yupo tayari hata kwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kuwa Curtis ni mtoto wake wa damu.
Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’.
Siwema ambaye Nay anadai kumfumania kitandani akiwa na mwanaume mwingine mjini Mwanza hivi karibuni, alisema Curtis si mtoto wa Nay, bali wa mwanaume mwingine ambaye hata hivyo hamtaji.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.
Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ na Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.
0 comments:
Post a Comment