2015-03-18

POLISI WAUA MGONJWA WA AKILI DALLAS, MAREKANI

 
Jason Harrison aliyeuawa na polisi kwa kupigwa risasi. 


Harrison akiwa amesimama mlangoni na bisibisi na polisi (kulia) akimwambia aitupe chini. 


…Akiondoka mlangoni ambapo polisi walimfyatulia risasi kadhaa. 


…Akiwa ameanguka baada ya kupigwa risasi. 


Huyu ni Shirley, mama yake Harrison. 


Huyu ni polisi John Rodgers wa Dallas ambaye amerejea kazini na mwenzake Andrew Hutchins.

VIDEO ya polisi wa Dallas, Marekani, wakimuua kwa risasi mgonjwa wa akili, Jason Harrison (39) Juni, 2014, imetolewa hivi karibuni. Video hiyo ilinasa tukio zima la kupigwa risasi kwa mtu huyo mbele ya mama yake mzazi akiwa na bisibisi.

Kwa mujibu wa tukio lenyewe lililotokea Juni 14, 2014, mama yake Jason aliwaita polisi kuja kusaidia kumdhibiti mwanaye huyo. Walipofika na kupiga hodi nyumbani hapo na yeye kuwafungulia mlango, polisi hao, John Rodgers na Andrew Hutchins, walimkuta Jason akiwa na bisibisi na hivyo kumtaka aitupe chini silaha hiyo na aliporudi nyuma, polisi mara moja wanampiga risasi. 

Mkanda huo unamwonyesha polisi mmoja akiwa na bunduki maalum ya risasi za kumpumbazisha mtu kiunoni mwake, lakini haikutumika kumdhibiti Harrison. Kilichofuatia ni kwamba Harrison anajikongoja hadi kwenye sehemu ya kuegesha gari akiwa amelowa damu na kuanguka huku mama yake akipiga kelele za “Mmemuua mwanangu!”

Polisi hao wanasemekana walimpiga risasi tano na pia familia hiyo imefungua kesi dhidi ya polisi hao ikisema Harrison hakuwa mtu mwenye vurugu na hakuwa tishio. Hata hivyo, mwanasheria wa polisi hao, Chris Livingston, amesema maofisa hao walikuwa wakilinda maisha yao na amesema kwamba kumuua mtu mwenye bisibisi ni rahisi sana kwa kutumia pigo moja tu.

Gazeti la Morning News limesema polisi walifanya hivyo katika kujihami kwani lilitokea haraka mno na kuwafanya wafanye walichokifanya.

Familia ya Harrison kupitia mwanasheria wake, Geoff Henley, imesema baada ya kuipata video hiyo, ni lazima yafanyike mabadiliko ya jinsi polisi wanavyopaswa kushughulikia watu wenye matatizo ya akili na si kukimbilia kutumia risasi.

Pamoja na polisi wa Dallas kukamilisha uchunguzi wa suala hilo na kulipeleka ofisi ya mwanasheria wa wilaya, mtandao wa Facebook umewalaumu polisi kwamba walimuua mtu huyo kimakosa. 
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...