Mtu mmoja amelipukiwa na simu yake ya iPhone 5C mfukoni katika mji wa New York nchini Marekani
Erik Johnson anayeishi katika kisiwa cha Long Island kilichoko kusini mashariki mwa New York alitoa maelezo huku akiwa na maumivu makali baada kuungua kwa miale ya moto ya simu hiyo.
Johnson alilazwa hospitali kwa siku 10 amesema kwamba alianza kuhisi kuungua kwa paja lake alipokuwa kwenye mazishi ya binamu yake.
Johnson alisema, ‘’Nilisikia sauti ya mlipuko kisha baadaye paja langu likaanza kuungua.
Kwa kawaida huwezi kutarajia tukio kama hilo kutokea na ni vigumu sana kuamini kilichotokea.’’
Johnson aliendelea kusema kwamba simu yake ya iPhone 5C iligoma kufanya kazi tena baada ya tukio hilo.
Kampuni ya Apple haijatoa maelezo yoyote kuhusiana na tukio hilo lililozuka katika kisiwa cha Long Island nchini Marekani.
Hapo awali, tukio hilo liliwahi kutokea lakini kampuni ya Apple haikutoa maelezo yoyote kuhusiana na kitendo hicho
0 comments:
Post a Comment