2015-03-19

Zao la muhogo linavyoweza kuwa na manufaa kiuchumi


  Mfanyabiashara katika Soko la Mgandini jijini Tanga, Hamis Mtote akionyesha mihogo aina ya Kibandameno ambayo inalimwa katika shamba la mfano lililoko Tarafa ya Maramba wilayani Mkinga.
Na Maimuna Kubegeya

Kadri siku zinavyozidi kwenda kumekuwepo juhudi za makusudi za uendelezaji wa zao la muhogo nchini.


Imeshuhudia taasisi kadhaa zinazojihusisha na kilimo zikitilia mkazo kilimo cha zao hilo na hata kuwafahamisha wakulimaa umuhimu wake.


Hivi karibuni Asasi ya Wanawake ya Kupambana na Umasikini (Iwapoa) na Umoja wa Wanawake Wanasiasa (Ulingo), iliendesha mafunzo ya matumizi ya unga wa muhogo kwa wanawake wa Wilayani ya Temeke ikilenga kuwakwamua kiuchumi kupitia zao hilo.


Kupitia mafunzo hayo, wanawake wakaelimishwa juu ya umuhimu wa zao la mhogo na kiwamba likitumika vizuri laweza kuwa na manufaa mengi kuliko aina nyingine za mazao na hasa ikizingatiwa kuwa bei yake ni nafuu.


Faida za muhogo


Wakufunzi mbalimbali waliweka bayana faida za zao hili, miongoni zikiwa ni majani yake kutumika kama mboga na kiazi chake, kutumika kama chakula kwa namna mbalimbali.


Katika viwanda, mazao yanayopatikana katika mzizi (mhogo), miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai. Baadhi ni vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki.


Vilevile, wanasema wanga wa muhogo hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari.


Unga wake nao hutumiwa kutengeneza vitu mbalimbali vikiwamo vitafunwa vinavyopendwa na watu wengi nchini.


Baadhi ya vitafunwa hivyo vinatajwa kuwa ni pamoja na keki, mikate, skonzi, biskuti na mandazi.


Umuhimu wa muhogo umekuwa ukiwachochea wadau wa kilimo nchini kuhakikisha kuwa zao hilo linatumika kuleta tija kwa mtu mmoja.


Wakufunzi wanaeleza kuwa muhogo kwa kawaida huchukuliwa kama zao la ziada lisilo la muhimu na ni jamii chache ambazo hulitegemea kwa chakula na biashara.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...