2015-02-03

Ni balaaaaaaaaa!!!!!!!!!!! Mawaziri wabanwa bungeni



Hata hivyo, hoja ya Lugola kuhusu Lukuvi na mwekezaji huyo ilipingwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alisema waziri huyo alisaidia hata kubadilisha mkataba wa umiliki wa Oystebay Villa, hivyo amwache.

Dodoma. Wabunge jana waliwaweka kitimoto mawaziri wanne wakiwataka watoe maelezo ya kukwama kwa baadhi ya mambo katika wizara zao na kusababisha matatizo kwa wananchi na Serikali kukosa fedha.

Mawaziri hao ni wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu; Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi, Waziri wa Maji; Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira. 


Wakichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji na ile ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, wabunge hao walionekana kukerwa na ahadi zisizotekelezeka za mawaziri hao kiasi cha wao kukata tamaa.

Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola akichangia taarifa hizo aliwashukia mawaziri watatu kwa wakati mmoja akieleza kuhusika kwao kukwamisha baadhi ya mambo.

Alisema migogoro ya ardhi nchini haitakwisha kama viongozi ndiyo wanaohusika kulinda baadhi ya watu. “Wako viongozi wanahodhi ardhi na kusababisha matatizo, mwekezaji wa Oysterbay Villa, Lukuvi ndiye alimsaidia kupata eneo alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Lugola na kuongeza:

“Sasa leo amekuwa Waziri wa Ardhi, itakuwaje? Mimi nitaichoma moto mbeleko inayombebea huyu mwekezaji kitendo kinachozuia Kinondoni kupata Sh3 bilioni. Huyu mwekezaji ana kiburi alizuia hata kamati kutaka kuingia kwenye eneo hilo lakini nikatumia ubaunsa wangu tukaingia.”

Hata hivyo, hoja ya Lugola kuhusu Lukuvi na mwekezaji huyo ilipingwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alisema waziri huyo alisaidia hata kubadilisha mkataba wa umiliki wa Oystebay Villa, hivyo amwache.

Lugola akiendelea kuchangia alimshukia Waziri Maghembe kwamba anapeleka maji katika eneo lake tu wakati wananchi wa jimbo la Mwibara na Bunda wakiteseka kwa mradi wao wa maji kutokukamilika.

“Waziri alisema uongo hapa kwamba mradi umekamilika kumbe ni uongo, niliwahi kuomba Rais atoe hawa mawaziri mizigo na nimefurahi amefanya mabadiliko hivyo naomba yawe ya tija,” alisema na kuongeza: “CCM isipigiwe kura hata mimi wasinipigie kama mradi wa maji hautakamilika.” 


Kuhusu Kilimo alieleza kuwa wanailinda Bodi ya Pamba na ndiyo maana kuna uchakachuaji mkubwa wa mbegu za pamba.

Alimtaka Nyalandu kwenda Mwibara kufanya mkutano na mamba na viboko ambao wanakula wapigakura wake huku akikaa kimya.

“Lazaro Nyalandu uende ukawazuie mamba na viboko na kama unataka kwenda Ikulu halafu umeshindwa kuzuia mamba je, ukiwa Ikulu utaweza kweli? alihoji Lugola.


Mwananchi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...