2015-04-08

Zari awatuliza wabaya wake............ni balaaaaaaaaaaaa

 
 MPENZI wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Dimond’, Zarinah Hassab ‘Zari The Boss Lady’, amewakata mdomo waliokuwa wakimbeza kuwa hana ujauzito kwa kuweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram akionyesha ‘kitumbo’ chake.

Watu mbalimbali walikuwa wakionyesha kutokuamini ujauzito wa mrembo huyo, huku wengine wakidai kuwa ni ya kutengeneza.

Msanii huyo wa Uganda, Zari, ambaye amekuwa kimya, juzi aliamua kuweka picha zake mbili kwenye mtandao wake wa Instagram, ambazo zilimuonyesha akiwa amelala katika kiti huku ‘kitumbo’ chake kikitokelezea.

Ingawa hakuweka ujumbe wowote kwenye picha hizo, lakini imeonekana kama alikuwa anajibu mapigo kwa wabaya wake.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...