NYOTA wa kike wa filamu nchini, Rose Ndauka, amesema pengo la msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba, litaendelea kuwepo kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye tasnia hiyo.
Wakati jana ikiwa ni kumbukumbu ya miaka mitatu tangu Kanumba afariki dunia, Rose alizungumza na MTANZANIA na kusema kwamba msanii huyo aliikuza tasnia hiyo kwa kutumia wasanii chipukizi, akishirikiana na nyota wengine wenye majina makubwa.
“Pengo la Kanumba litaendelea kuwepo na tutazidi kumkumbuka, kwani alipenda kuona kila msanii chipukizi anafanya vizuri, lakini kwa sasa tasnia hii inayumba kwa kukosa ushirikiano na ushindi ambao ulikuwa ukiletwa na mwenzetu,” alisema Rose, akiongeza kwamba tangu Kanumba afariki hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea.
0 comments:
Post a Comment