MSANII wa filamu pamoja na muziki, Baby Madaha, amesema sanaa ya sasa inatakiwa kuwa na ubunifu, ili kuweza kufikia katika kiwango cha juu.
Akizungumza na MTANZANIA, Madaha alisema asilimia kubwa ya wasanii wanakuwa hawana ubunifu katika sanaa, kitu ambacho kinawafanya washindwe kufanya vizuri.
“Mashabiki wetu wameendelea sana na wanajua kitu bora na magumashi. Hivyo kwa sasa tunatakiwa tuendeleze ubunifu ili kuweza kuwagusa mashabiki wetu na hata kuwafikia wenzetu wa nje,” alisema.
“Sanaa ya sasa siyo ya kuingia kichwa kichwa, ndiyo maana baadhi ya wenzetu wanaingia kwenye tasnia kupitia sehemu kama THT na Bongo Star Search ili kujipika vizuri.”
0 comments:
Post a Comment