2015-04-10

Dimpozi: Nje nafuata fedha, mzimu wangu upo bongo


MSANII wa bongo fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ameweka wazi kwamba huwa anakwenda katika maonyesho nchi za nje kwa sababu ya fedha, si mapenzi na nchi hizo.

Amesema hata akifika katika nchi hizo huwa anatamani kurudi mapema Tanzania, jambo ambalo huwa linamshangaza kila wakati.


Msanii huyo aliliambia MTANZANIA kwamba kinachompa kiburi cha kuendelea kufurahia nchi hii ni kutokana na amani na uhuru anaoupata, tofauti na anapokuwa katika maonyesho yake nchi za nje.

“Nimekuwa nikiandamwa na mzimu wa kukumbuka nyumbani, hivyo ndivyo ninavyoweza kusema, asikwambie mtu, nyumbani ni nyumbani, hata kama nje kuna raha kiasi gani,” alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz ameendelea kufanya vizuri kupitia wimbo na video yake ya ‘Wanjera’, ambao video yake imeshirikisha watu mbalimbali maarufu, akiwemo mwigizaji Wema Sepetu na mshindi wa Big Brother Africa (BBA) mwaka jana, Idriss Sultan.

Breaking News!!! Mabomu ya Machozi yanarindima muda huu Kituo cha Mabasi Ubungo hali mbaya mgomo wa madereva


Katibu wa Madereva Mboka akiongea na wandishi wa Habari muda huu, kabla ya mabomu hayajarindima

…Mgomo wa Mabasi kuwa endelevu hadi watakapo achiwa viongozi wao wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi

Na Andrew Chale wa Modewji blog

Modewji blog ambayo imepiga kambi katika kituo cha Mabasi Ubungo kuanzia majira ya saa 11, alfajiri, ni kuwa tayari baadhi ya viongozi wa madereva wametoa tamko rasmi kuwa mgomo wao huo utaendelea hadi hapo viongozi wao wakuu zaidi ya Sita (6) wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi watakapoachiwa huru ikiwa ni pamoja na kuondoa masharti dhidi ya waliyowekewa katika suala la leseni kwa madereva hao.

Kwa mujibu wa Katibu Mwenezi wa madereva, Mboka Mwalaikwe alibainisha kuwa suluhu pekee kwa kunusuru abiria waendelee na safari ni kwa Jeshi la Polisi kuwaachia huru viongozi hao wanaowashikilia.

“Huu sio mgomo bali ni kueleza kwamba baadhi ya mambo wanayotufanyia Serikali sasa yamefika mwisho, Aprili Mosi mwaka huu tulitaangaza rasmi kuwa ifikapo Aprili 10, endapo madai yetu ya msingi hayajatatuliwa basi tutagoma. 

Baadhi ya madereva wakiwa wamejikusanya muda huu huku magari yaakiendelea kuwashwa moto

Hata hivyo Jana Aprili 9, Jeshi la Polisi asubuhi limewakamata viongozi wetu sita akiwemo Mwenyekiti, msaidizi na wajumbe wake na kuwashikiria, hii bado si haki na sisi tutaendelea na mgomo huu kwanza hadi waachiwe na pia waje hapa watu wa NIT, Waziri na Jeshi la Polisi kwani wao ndio wanasababisha matatizo makubhwa” alieleza Mboka.

Kwa upande wao badhi ya madereva walioongea na Modewji blog, walieleza kuwa, wamechoka na unyanyasi unaofanywa na Serikali ikiwemo kupitia idara na taasisi zake kwani zinaanzisha mambo makubwa ambayo utekelezaji wake ni mgumu pia inawakandamiza wao madereva.

Mabomu mabomu mabomu ya machozi yanapigwa muda huu hapa standi ya mabasi Ubungo hali ni mbaya… 




TAFADHALI TAARIFA HIZI UKINAKILI KWENYE CHOMBO CHAKO UTAJE UMEZIPATA MODEWJI BLOG!!!!

WANDISHI WA HABARI WOTE WANAPIGWA HUKU HAKUNA ANAYEPONA WATU WOTE WAMETAKIWA KUTOKA NJE YA STAND NA NJE MAGARI YANA YANACHOMWA MOTO HASA NOAH ILIYOTAAKA KUBEBA ABIRIA… PICHA NA TAARIFA ZAIDI ZINAWAJIA PUNDE TENA MAANA HAPA NILIPO NIMELEWA MOSHI WA MABOMU…
 MODEWJIBLOG.

KADJA: KWA MAISHA HAYA MUME WA NINI?


Staa kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Khadija Maige ‘Kadja Nito’. 

STAA kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Khadija Maige ‘Kadja Nito’, hatimaye ameamua kufunguka na kusema kuwa, kwa maisha yake ya sasa ya kimuziki haoni kama kuna umuhimu wa kufikiria masuala ya kuolewa.

Akizungumza na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Kadja alisema kuwa, muziki sasa ndiyo kila kitu kwake hivyo hawezi kumpa nafasi mwanaume au kuzungumzia suala la ndoa hivi sasa. 

“Naweza kuishi maisha yangu bila mwanaume, napata mshiko, nawasaidia ndugu zangu na mimi najimudu, mume wa nini maisha haya? Sasa ni muziki na mimi, mimi na muziki, mapenzi yasubiri,” alisema Kadja.
GPL

ALA KICHAPO TAKATIFU KISA MUME WA MTU


Jamila akiwa na jeraha usoni kwa tuhuma zakutembea na mume wa mtu.
 
Dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Jamila mkazi wa Kawe jijini Dar hivi karibuni alipata kipigo cha kufa mtu akituhumiwa kuchepuka na mume wa mwanamke mmoja aitwaye Sheila.Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa, Sheila alitonywa na wambeya kuwa Jamila amekuwa akichepuka na mumewe na bila kuchunguza akapanga kumshikisha adabu.

“Jamila alikuwa akituhumiwa kutembea na mume wa Sheila na siku ya tukio alifuatwa baa na kupigwa hadi kutaka kutobolewa jicho,” kilidai chanzo. 

Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwatafuta wahusika ambapo Jamila alipopatikana alisema:
“Jamani ukweli ni kwamba mimi niliwahi kutembea na yule mume wa Sheila lakini tulishaachana sasa nimemshangaa mkewe kuja na kunipa kipigo sababu tu ya maneno ya kusikia”, alisema Jamila na kuongeza: 


                      Mwenye mume.

“Nilikwenda kufungua kesi Kituo cha Polisi Kawe lakini siku chache baadaye Sheila alikuja na kuniomba msamaha akidai kuwa alikoasea kuamini maneno ya watu bila kufanya uchunguzi. Tumesameheana na yameisha.”
GPL

Aliyekuwa Mke wa Mh Mbunge Sugu, Faiza Ally Atangaza Mtandaoni Kuwa Ana Hamu ya Kufanya Mapenzi......Kazi Kwenu Wanaume



Mrembo asiyeishiwa vituko, Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ ametoa kali baada ya kusema kuwa ana hamu ya kumpata mwanaume mwingine wa kumpa raha lakini mpaka sasa hajapata.

Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram, Faiza alisema tangu alipoachana na Mheshimiwa Sugu, aliona bora ajitulize lakini sasa anajiona kuna kitu anakikosa na wa kumpa kitu hicho ni mwanaume.



“Niseme tu kwamba tangu niachane na Sugu sijakutana na mwanaume mwingine, hebu ‘imagine’ ni muda gani? Sasa nimeshindwa kuvumilia, natafuta wa kunipa raha maana kuna hali flani ikinijia nakuwa kama chizi, swali ni je, nani mwanaume sahihi wa kunipa ‘zawadi’ hiyo? Hapo ndipo mtihani ulipo,” alisema Faiza.

Zitto Kabwe Asema Kitendo Cha kuitwa MSALITI Ni Mbinu Zinazotumika Kumuua Mwanasiasa wa Upinzani

Kiongozi wa chama cha ACT-Tanzania,Zitto Kabwe amesema kuitwa msaliti ni mbinu zinazotumika 'kumuua' mwanasiasa wa upinzani nchini.

Amesema mwanasiasa wa upinzani akitakiwa kuuawa kisiasa si jambo geni kusikia anatuhumiwa kutumika na Usalama wa Taifa au Pandikizi la Chama cha Mapinduzi, CCM.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dae es Salaam juzi,Zitto alisema kauli kama hiyo ilitumika kumshusha kisiasa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Mabere Marando na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

"Si jambo jipya, mmesahau kwamba Mbatia aliitwa pandikizi,leo Mbatia yuko wapi,si yuko meza moja na UKAWA?

"Mmesahau baada ya serikali ya Umoja wa kitaifa juzi tu hapa kwamba CUF waliitwa CCM-B, mmesahau kwamba CUF waliitwa mashoga, leo kiko wapi?

"Mmesahau Marando aliitwa pandikizi, tena dhidi ya Mrema(Mwenyekiti wa TLP),leo Marando ni shujaa na Mrema tunamtukana.Hizi ni siasa tu na zitaendelea tu," alisema

Aidha alisema kuna watu wengine wataibuka baadaye nao wataanza kulaumiwa, kama Mwalimu Nyerere alivyosema.....Ukishakula Nyama ya Mtu Huachi.

Kutokana na hali hiyo alisema, walioitwa wasaliti wametoka huko walikokuwa na watasikika wasaliti wengine wanaibuka kwa sababu siasa iko hivyo..

"Juzi nimemsikia Halima Mdee anasema mimi siyo ACT,ninyi mliwahi kuandika kama Halima ni ACT,hiyo maana yake nini,inamaanisha kuna presha anapigwa huko.

"Angalau Shibuda ni mtu ambaye haeleweki misimamo yake ni nini, lakini hivi ni vitu vya kawaida,"alisema.


Akizungumzia kutumiwa na vyombo vya usalama,Zitto alisema yeye kama kiongozi hawezi kuacha kuwasiliana na watu wa usalama wa Taifa.

"Huwezi kuwa kiongozi wa chama kikubwa kinachojiandaa kushika dola usiwe na uhusiano na Mkuu wa Jeshi la Polisi,Mkuu wa jeshi la wananchi au Mkuu wa Usalama wa Taifa,utakuwa ni kiongozi wa ajabu sana." Alisema

Askari wa JKT Auawa Wakati Akisaidiana na Polisi Kuyakabili Majambazi Yaliyokuwa Yamepora Fedha Iringa


Watu wawili akiwemo jambazi mmoja na askari mwanafunzi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamekufa na wengine kunusurika kuuawa katika tukio lililotokea juzi, mjini Mafinga mkoani Iringa wakati majambazi wakirushiana risasi na askari wa Jeshi la Polisi.

Risasi hizo zilipigwa wakati Polisi hao wakijaribu kuokoa fedha za mfanyabiashara Salama Semwaiko zilizoporwa na majambazi wawili waliotumia pikipiki wakati wakifanya uporaji huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema mfanyabiashara huyo aliporwa fedha hizo juzi majira ya saa 2.45 asubuhi alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda kwenye biashara zake.

Tukio hilo la kusikitisha lililovuta hisia za watu wengi na kufanya baadhi kuzimia wengine kukimbia hovyo na kujifungia ndani kwa ajili ya kuokoa maisha yao lilitokea katika eneo la Kinyanambo B, nje kidogo ya mji wa Mafinga.

Kamanda Mungi alisema; “mfanyabiashara huyo akiwa katika gari lake akielekea kwenye biashara zake mjini Mafinga, mfanyabiashara huyo alisimamishwa na mtu mmoja aliyekuwa amevaa koti jeusi na baada ya kusimama alimtolea silaha na kumtaka atoe fedha na vitu vyote vya thamani alivyokuwa navyo .” 

“Baada ya kuona hana msaada mfanyabiashara huyo alijikuta akilazimika kutoa Sh 700,000 alizokuwa nazo, simu ya mkononi na baadaye ilitokea pikipiki ambayo haikufahamika namba za usajili na kumpakia mtu huyo na kuanza kukimbilia eneo la Kinyanambo,” alisema.

Alisema mara baada ya majambazi hao kutoweka, Jeshi la Polisi lilipewa taarifa na kuwahi eneo la tukio na kwa kushirikiana na wananchi walianza kuwakimbiza majambazi hao na ndipo majibizano ya risasi yalipoanza. 

Katika hekaheka hiyo, Kamanda Mungi alisema Said Ngudi (25) ambaye ni askari wa JKT Makutupora, Dodoma alipigwa risasi na kufa papo hapo wakati akisaidia kupambana na majambazi hao.

Diwani wa CHADEMA Apewa Adhabu ya Kufua Shuka za Wagonjwa Hospitalini na Kuzibua Mitaro ya Barabarani


Diwani wa Kata ya Kasanda wilayani Kakonko, Dickson Barutwa (40) wa Chadema na wenzake watatu, wamehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kibondo adhabu ya kufua shuka za wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kakonko na kuzibua mitaro ya barabarani kwa siku 14 baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu.

Baadhi ya makosa hayo yametajwa kuwa ni kuifunga ofisi ya Mtendaji wa Kijiji isivyo halali na kuweka gundi na unga wa ngano kwenye kufuli kwa lengo la kumzuia Mtendaji wa Kijiji asifanye kazi.

Mbali ya Barutwa wengine ni Daudi Obadia (32), Hatari Kasase (33) na Brighton Jona(29), wote wakazi wa kata ya Kasanda, Kakonko. 

Watu hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibondo, Erick Marley na kusomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Peter Makalla.

Mwendesha Mashtaka alisema mnamo Novemba 8 mwaka jana, majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha Kaziramihunda, watuhumiwa wote kwa pamoja walifika katika ofisi ya Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho isivyo halali na kuifunga ofisi hiyo kwa kuweka gundi aina ya Super Glue na unga wa ngano kwenye kufuli ili kumzuia Mtendaji asifanye kazi yake.

Inadaiwa watu hao walifikia uamuzi huo kwa madai kuwa hawakuwa wanamtaka Mtendaji huyo wa Kijiji, Amos Peter na kumtishia kumuua.

Kutokana na makosa hayo, Mahakama ya Wilaya ya Kibondo imewahukumu kulipa faini ya Sh 50,000 au kufungwa jela miezi mitano kwa kosa la kufunga Ofisi ya Mtendaji, na pia kulipa faini ya Sh 50,000 au kwenda jela miezi miwili kwa kosa la kufanya fujo. 

Watuhumiwa wote walilipa faini na kuachiwa huru isipokuwa Kasase anayekabiliwa na kesi nyingine ya mauaji, hivyo alirudishwa gerezani.

Aidha, katika kosa la kutishia kuua diwani huyo na wenzake watatu wamehukumiwa adhabu ya kazi za kijamii ambayo ni kufua shuka za wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kakonko kwa muda wa wiki moja na kuzibua mitaro ya barabara kwa muda wa wiki moja pia.

Tayari diwani huyo na wenzake wameshakabidhiwa katika Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuanza adhabu hiyo. Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo walioachiwa huru baada ya kukutwa hawana hatia, ni Boniface Obadia (35) Amos Buseni (33), Majaliwa Charles (24) na Samora Barichako (35), wote wakazi wa kijiji cha Kaziramihunda.

Huyu Ndo Mtanzania Anayetuhumiwa Kwa Ugaidi Kenya.....Jana Alifikishwa Mahakamani Chini Ya Ulinzi Mkali


Mtanzania anayedaiwa kuhusika katika shambulizi la kigaidi lililoua watu 148 katika Chuo Kikuu cha Garissa – Kenya, Rashid Charles Mberesero, jana alifikishwa mahakamani na kuwekwa kizuizini kwa mwezi mmoja wakati polisi wakiendelea kukusanya ushahidi dhidi yake.

Mtuhumiwa huyo ambaye pia anafahamika kwa jina la Rehani Dida alirejeshwa Nairobi kutoka Garissa alikopelekwa awali kwa ajili ya kuhojiwa baada ya kukiri kujihusisha na kundi la Al- Shabaab.

Mahakama jijini Nairobi ilisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ambaye hakutakiwa kujibu tuhuma hizo na wenzake wanne watalazimika kuwa chini ya uchunguzi mkali wa polisi kwa kipindi cha mwezi mmoja na baadaye wanaweza kusomewa mashtaka ya kuhusika katika shambulizi hilo lililoua watu hao, wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

Haikufahamika mara moja sababu za kuamuliwa kuwekwa kizuizini kwa muda huo mbali ya taarifa kueleza kuwa ‘watashikiliwa na polisi tena katika kituo cha siri’.

Mwendesha Mashtaka, Daniel Karuri aliiambia Mahakama hiyo kuwa Mtanzania huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano, alikuwa amepanga safari ya kuelekea Somalia kwa ajili ya kujiunga na makundi ya kigaidi.

Watuhumiwa hao ni kati ya 14 waliotiwa mbaroni hivi karibuni baada ya shambulizi hilo la kigaidi.

Mahakama hiyo pia imewaamuru washukiwa wengine kuendelea kushikiliwa na polisi kwa muda wa siku tano hadi 15.

Awali, Karuri aliiambia Mahakama hiyo kuwa polisi walikuwa wakifuatilia kwa karibu uhusiano baina ya wale waliofanya shambulizi hilo na mfanyabiashara mmoja anayemiliki hoteli mjini Garissa. Inasemekana kuwa watu waliotekeleza shambulio hilo walikuwa wamelala katika hoteli hiyo.

Hakula chakula cha shule
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kigwe, mkoani Dodoma alipokuwa akisema Mberesero baada ya kufaulu kutoka Gonja, wamesema hakuwahi kula chakula chochote shuleni kwa kipindi cha mwezi mmoja aliokaa akisubiri kuhamishwa na kubadilishiwa mchepuo wa masomo.

Wakizungumza na mwandishi wetu shuleni hapo jana, wanafunzi wa kidato cha tano, Yoram James na Thomas Godwin, walisema siku zote alizoishi shuleni hapo alikuwa akila kwa mama lishe jirani na shule hiyo.

“Lakini alikuwa na mkarimu kwetu wakati mwingine alikuwa akitununulia maandazi ya kunywea chai,” alisema Yoram.

Hata hivyo, walisema kutokana na upole wake, jinsi anavyoongea na kutumia muda mrefu msikitini, walimpa jina la Ustaadhi.

“Alikuwa akienda mjini mara kwa mara, nadhani alikuwa akiomba ruhusa kwa walimu au alikuwa akitoroka,” alisema Thomas.

Thomas alisema Rashid alikuwa akipenda kucheza mpira wa miguu kwa hiyo alitenga muda wake kwa ajili hiyo.

Uhamisho wake
Mkuu wa Shule hiyo, Ramadhan Bakari alisema ofisi ya elimu mkoa ilituma taarifa ya kuwataka wanafunzi wanaopenda kubadilisha mchepuo kuandika barua ya maombi.

“Rashid alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi watano walioomba kubadilishiwa mchepuo kutoka Sanaa kwenda Sayansi, walikubaliwa wanne akiwamo yeye,” alisema Bakari.

Hata hivyo, mwalimu huyo alisema Rashid alikuwa akihangaika ahamishiwe Shule ya Sekondari ya Bihawana, tangu aliporipoti Kigwe.

“Hatuwezi kuzungumza kuhusu tabia zake maana hapa hakuishi siku nyingi, alikuwa kama yuko njiani,” alisema.

“Aliondoka hapa shuleni kwenda Bihawana Agosti 19, mwaka jana baada ya taratibu kukamilika,” alisema.

Uvumi wasambazwa
Hofu imetanda katika maeneo mbalimbali baada ya kusambazwa ujumbe kwenye simu na mitandao ya kijamii ukidaiwa kutolewa na Umoja wa Mataifa (UN) kutahadharisha watumishi wake waepuke kukaa katika makundi makubwa na mikusanyiko katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha leo kuepuka mashambulizi ya kigaidi.

Hata hivyo, Msemaji wa UN, Usiah Ledama alikanusha umoja huo kuhusika na ujumbe huo akisema ni feki na hauna ukweli wowote.

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Diwani Athumani alisema hata kama ujumbe huo ni feki, bado Jeshi la Polisi linachukua tahadhari kuhakikisha Taifa linakuwa salama.

“Huo ujumbe uwe feki au wa kweli, lazima tuchukue tahadhari, Tanzania si kisiwa, tutakuwa salama kwa asilimia 100, kwa hiyo ulinzi unaimarishwa,” alisema.

Alisema ni lazima kila mtu awe mlinzi wa mwenzake na ahakikishe kuwa anakuwa mzalendo kwa kutoa taarifa zozote ambazo anadhani zitalisaidia Jeshi la Polisi katika ulinzi.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Arusha Akanusha Kukamatwa Kwa Mwanaume Mwenye Mabomu Na Watu Wanne Wenye Bunduki



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatusi Sabas amekanusha uvumi ulioenea katika mitandao ya jamii kuhusu kukamatwa mwanaume mmoja aliyevalia vazi la baibui akiwa na bomu mkoani humo na kwamba watu wengine wanne wamekamatwa wakijiandaa kuingia chuo cha uhasibu.

Uvumi huo umeanza kusambaa kwa kasi leo asubuhi ukidai kukamatwa kwa watu wanne waliokuwa ndani ya gari aina ya Toyota Premio huku wakiwa na bunduki 4 aina ya SMG na Risasi 160. 

Ujumbe huo ulidai kuwa watu hao walikamatwa jana usiku wakijiandaa kuingia chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kuonana na ndugu yao mmoja wa kike anayeishi katika hosteli za chuo hicho.

Pia ilielezwa kuwa, baada ya kufika getini,mlinzi aliwashtukia na kupiga simu polisi ambapo walikamatwa. 

Mbali na taarifa hizi kukanushwa na kamanda wa Polisi,Mpekuzi imeongea na Raisi wa wanafunzi wa Chuo hicho ndugu Iman Mkumbo ambaye naye amezikanusha taarifa hizo na kusema si za kweli.

"Hali ni shwari hapa chuoni,tangu juzi usiku kuna doria kali ya polisi maeneo yote ya chuo, hivyo watu wanapata hofu na kuanza kuzusha taarifa zisizo za kweli."Amesema Mkumbo

Sakata la Gwajima: Polisi Wamhoji Kwa Masaa Matano..... Atakiwa Kurudi Polisi Wiki Ijayo na Hati ya Usajili wa Kanisa Lake,Helkopta na Viwanja Anavyomiliki


Askofu wa Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima amelitikisa tena Jiji la Dar es Salaam jana mara baada kuwasili makao makuu ya Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili kuendela na mahojiano kuhusu tuhuma za kumkashfu Askofu Pengo.

Gwajima aliwasili Makao Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake .

Eneo lote la kituo hicho cha polisi lilikuwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.

Baada ya kuwasili kituoni hapo, umati mkubwa wa Waumini wake ulizunguka maeneo yote ya Kituo hicho huku wengine wakiwa maeneo ya stendi ya Treni ya Reli ya kati.

Kama kawaida, Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa mahususi kumpa nguvu Askofu huyo ajibu kesi hiyo kwa ufasaha. 

Baada ya Mahojiano ya takribani masaa Matano, hatimaye Askofu Gwajima alitoka ndani ya kituo hicho,lakini katika hali isiyo ya kawaida,Askofu huyo aligoma kuongea na vyombo vya habari.

Baada ya Gwajima kugoma kuongea,mwandishi wetu alimfuata Mwanasheria wake aliyekuwa ameambatana naye,John Mallya ambaye alisema kuwa mteja wake alikuwa amechoka, hivyo asingeweza kuongea.

Mallya alimweleza mwandishi kuwa mambo aliyohojiwa Gwajima ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu Pengo.

“Mahojiano yamekwenda vizuri lakini nasikitika sana kutokana na mambo waliyokuwa wanamhoji. Wamemuuliza mambo ambayo hayahusiani kabisa na kile tulichotarajia na ndicho kilichotuleta hapa, nilidhani mteja wangu ataulizwa kuhusiana na matumizi ya lugha chafu iliyodaiwa kutumika kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini,” alihoji wakili wa Gwajima. 


Aliendelea kusema kuwa, mambo aliyoulizwa ni kuhusiana na ukoo wake, wazazi wake hata ndugu zake na watu wengine wa kwao waliokufa.

Alisema walihoji pia juu ya mambo mengine kama umiliki wa helikopta, utajiri wake, nyumba anayoishi, uhusiano wake na watu mbalimbali.

“Nimeshangaa sana kuona mteja wangu ameulizwa vitu kama hivyo ambavyo havihusiani na madai ya hapo awali ya matumizi ya lugha ya matusi. Tumeagizwa tulete nyaraka kumi siku ya mahojiano yetu tena yatakayofanyika tarehe 16 mwezi huu na sisi tutafanya hivyo,” alisema Mallya.

Alizitaja nyaraka na vitu vingine wanavyotakiwa kuvipeleka Aprili 16 ni hati ya usajili wa kanisa, bodi ya udhamini wa kanisa na majina yao, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake, na muundo wa uongozi wa kanisa lake.

Vingine ni namba ya usajili wa kanisa, ritani za kanisa lake (mapato na matumizi ya fedha za kanisa lake), mtu anayechukua na kurekodi mkanda wa video kanisani kwake, pamoja na waraka wa Baraza la Maaskofu uliosomwa makanisani.

GWAJIMA AWAACHA WAUMINI WAKE NJIA PANDA


Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewaacha waumini wake njia panda kufuatia kauli yake ya kuwataka wamsindikize Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati jijini Dar, jana alipokwenda kuhojiwa huku Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwa ametoa tamko la kuzuia waumini hao kukusanyika kituoni hapo. 

Gwajima aliyetoa kauli hiyo kwa waumini wake katika ibada ya Jumapili iliyopita kanisani kwake, Kawe jijini Dar, alitarajiwa kufika kituoni hapo kujibu tuhuma za kumtusi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinari Pengo.

Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa majina yao, juzi jijini Dar, baadhi ya waumini wa Gwajima walisema wanashindwa kufanya uamuzi wa kumsindikiza kiongozi huyo kwani jeshi la polisi limesema halitaruhusu mtu kumsindikiza.

“Kusema kweli tumebaki njia panda maana mchungaji amesema twende tumsindikize lakini Kova naye kasema jeshi la polisi litatumia nguvu kuwatawanya watu ambao watakaidi amri hiyo ya jeshi la polisi,” alisema muumini mmoja huku waumini wenzake wakiunga mkono. 


Wakati Gwajima alipowataka waumini wake wamsindikize kituoni hapo, Kova alisisitiza kuwa kiongozi huyo wa dini anatakiwa kufika kituoni hapo akiwa na mwanasheria wake pamoja na watu wachache tu wa karibu hivyo kuwafanya waumini wengi wa kanisa la Gwajima kubaki njia panda.

Kupitia video inayomuonesha Gwajima akimtupia maneno makali Pengo, mchungaji huyo wa Ufufuo na Uzima alimtuhumu Pengo kuwa amewasaliti maaskofu wenzake waliotoa tamko la kuipigia kura ya ‘Hapana’ Katiba Inayopendekezwa kwa kile walichodai haikukidhi matakwa ya wananchi.
GPL

SAJENT; ETI SASA VIMINI PEMBENI, SWALA NA YEYE!


Mwanadada muigizaji Husna Idd ‘Sajent’.
 
Kama kawa, kama dawa leo kupitia safu hii tunaye mwanadada muigizaji Husna Idd ‘Sajent’. Wengi wanataka kujua siri ya ukimya wake hivyo mwandishi wetu Hamida Hassan alimtafuta na kumpiga maswali 10 kama ifuatavyo.

Ijumaa: Husna, siku hizi huonekani kabisa kwenye anga za starehe, ni kwa nini? Au ndo tuseme umefulia?
Sajent: Sajent wa sasa si yule watu waliyemzoea, nimeamua kuishi maisha ya tofauti kabisa ndiyo maana siyo mtu wa kujiachia kivile. 

Ijumaa: Kuna habari kuwa umeolewa na msanii mwenzako Gabo na ndiyo maana hata mfumo wako wa maisha umebadilika, hilo unaliongeleaje?
Sajent: Watu wanapenda sana kuongea, acha waongee kwani siwezi kuwabadili lakini mimi na Gabo tuko karibu sana, nampenda kama msanii mwenzangu.

Ijumaa: Je, una mchumba kwa sasa? Na kama yupo, mipango ya wewe kuingia kwenye maisha ya ndoa ikoje?
Sajent: Ni kweli mchumba ninaye na Mungu akipenda nitaolewa tu.

Ijumaa: Inaweza kuwa mchumba ndiye kakubadilisha mpaka sasa huonekani na vimini kama zamani bali ni mtu wa madira kila wakati?
Sajent: Nikiri tu kwamba mchumba wangu ndiyo chanzo cha mabadiliko ya maisha yangu, amekuwa akiniongoza kumjua Mungu zaidi.

Ijumaa: Katika siku za hivi karibuni umekuwa ukionekana una mimba na hata mashosti zako walieleza kuwa, una kitumbo, hebu funguka. 

Sajent: Mh! Watu bwana, kile kitumbo ilikuwa filamu bwana. Filamu yenyewe inaitwa On Set, watu wataiona tu.
Ijumaa: Mbona inadaiwa ulikuwa nayo ukaitoa?
Sajent: Sijawahi kutoa mimba, naanzaje kufanya tukio hilo la kinyama jamani?
Ijumaa: Huyo mchumba wako anapokutembelea huwa unapenda kumpikia chakula cha aina gani?
Sajent: Mchumba wangu ni mpenzi sana wa wali samaki, hivyo akisema tu anakuja siku hiyo natulia na kumpikia ile kitu roho yake inapenda.

Ijumaa: Wewe ni muislam, kuna wakati kweli unamkumbuka mola wako?
Sajenti: Kama nilivyosema awali, sasa hivi nimebadilika na kwa kweli najitahidi kusali sala tano.
Ijumaa: Ukiwa home unapenda kufanya nini hasa?
Sajent: Ni kazi za nyumbani kama mwanamke lakini nikiwa free napenda kujisomea Quran.

Ijumaa: Ni tabia gani za mastaa wenzako ambazo zinakukera?
Sajent: Majungu, umbeya, kuchukuliana mabwana, mabifu yasiyokuwa na maana ni kati ya tabia zinazonichefua.
GPL

PENZI LA NAY, SHAMSA SIWEMA, MUME WA SHAMSA VILIO

 Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego na Shamsa Ford wakipozi kimahaba.
Penzi matata linalowanyima usingizi baadhi ya watu mjini kwa sasa kati ya mwigizaji wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ limeibua tafrani kubwa huku waliokuwa wapenzi wa mastaa hao wakijikuta wakiangua vilio kweupe, Ijumaa limesheheni.

TATIZO MAHABA NIUE
Mara baada ya wawili hao kutangazwa rasmi kuwa sasa ni mahaba niue huku picha za ushahidi zikimwagwa, aliyekuwa mwandani wa Nay, Siwema a.k.a Wemalicious na aliyekuwa mume wa Shamsa, Dickson ‘Dick’ wanadaiwa kujikuta kwenye hali mbaya kiasi cha kumwaga machozi.

TUJIUNGE NA CHANZO KWA SIWEMA
Habari kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Siwema jijini Mwanza zilidai kwamba, mara baada ya picha za wawili hao kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii aliumia roho hasa alipomuona Shamsa akijiachia kwenye nyumba ambayo alishirikiana na Nay kuijenga.

“Yaani Siwema ameumia hadi akajikuta akiangua kilio kwa uchungu. Sikukuu ya Pasaka ilikuwa mbaya kupita kiasi kwa Siwema. “Kinachomuuma zaidi ni kwamba hata nguo zake za mtoko Shamsa anavaa ‘gym’ na kufanyia mazoezi. Jamani kuna dharau zaidi ya hiyo? “Ukweli roho inamuuma vibaya mno,” kilisema chanzo hicho kwa ombi la kutochorwa jina gazetini. 


Ney na Shamsa wakifuatilia jambo kwenye simu.

Kabla ya kuhamia kwa chanzo cha mume wa Shamsa ili kupata ubuyu kamili, gazeti hili lilimsaka Siwema ili kujua anachukuliaje jambo hilo ambapo alifunguka ya moyoni.

SIWEMA AANIKA MAZITO
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu kutoka jijini Mwanza, Siwema mwenye mvuto wa kuvunja midume shingo alianika mazito kwamba, kitendo cha Nay kumuacha na muda si mrefu kwenda kwa Shamsa ni upuuzi.

Siwema alifunguka kwamba, kinachomshangaza ni kitendo cha Shamsa kuvaa nguo zake na kufanyia mazoezi.

Mwanamama huyo alisema watu watamtukana kwa kuwa hawajui tabia ya Nay kwani hata Shamsa atamshindwa tu.

“Nilivumilia vitu vingi sana. Maumivu nayajua mimi, nyumba tuliyojenga wote, anaingia mwanamke mwingine. Namhurumia sana Shamsa kwani hajui tabia za Nay,” alifunguka mtoto mweupe, Siwema kwa uchungu.

KUMBE SIWEMA ALIJUA
Habari zilieleza kwamba, Siwema alijua muda mrefu kuwa Nay anatembea na Shamsa lakini alipomuuliza staa huyo anayetamba na Ngoma ya Akadumba alimwambia walishaachana. 


                                     Siwema.

NAY ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo, Nay alisema kuwa yeye yupo na Shamsa na kwamba anamshangaa huyo Siwema kwani alishaachana naye.

TUJIUNGE NA CHANZO KWA MUME WA SHAMSA
Kwa mujibu wa chanzo makini, naye kama Siwema, baada ya penzi la Shamsa na Nay kuwa ndiyo habari ya mjini huku wakitupia picha za malovee mtandaoni, mume wa Shamsa, Dick alipaniki kiasi cha kutokwa machozi huku akitafuta namna ya kupooza machungu.

JB AOMBWA AOKOE JAHAZI
Habari zilidai kwamba, Dick alikimbilia kwa staa wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ na kwenda kumuomba aokoe jahazi akimshitakia Shamsa kuwa ameamua kumwacha na kuamua kutembea na Nay, jambo ambalo analiona kuwa ni udhalilishaji kwani ni mkewe ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Terry. 


Mwanamuziki kinara wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Ilidaiwa kuwa, baada ya Dick kufika nyumbani kwa JB maeneo ya Ubungo-Kibangu, Dar na kumweleza hayo, mwigizaji huyo alimpigia simu Shamsa ambaye humwita Daddy na kumuuliza juu ya suala hilo ambapo alimweleza kuwa alishaachana na Dick hivyo kila mmoja ana maisha yake.

Katika hali hiyo, JB aliwataka kukaa chini na kuyamaliza kiutu uzima kuliko kuwekeana kinyongo.

SHAMSA ANASEMAJE?
Baada ya kusikia kilichopo upande wa mume wa Shamsa, gazeti hili lilimgeukia Shamsa na kumwelezea kila kitu kilichopo ambapo alionesha kumshangaa Dick kwa kuwa alishamalizana naye tangu Oktoba, mwaka jana.

“Kwanza namshangaa kwa nini anawaka wakati kila mtu ana maisha yake?“Tulishaachana tangu mwaka jana so kila mtu ana maisha yake,” alisema Shamsa ambaye kwa sasa amehamishia moyo wake kwa Nay. 


Aliyekuwa mume wa Shamsa, Dickson ‘Dick’.

DIAMOND ACHAFUA HALI YA HEWA
Wakati sakata la Shamsa na Nay likishika kasi mithili ya moto wa kifuu, mwanamuziki kinara wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amechafua hali ya hewa baada ya kutundika mtandaoni picha ya mahaba ya wapenzi hao iliyosababisha tafrani zaidi.

Diamond ambaye ni swahiba wa Nay ndiye aliyekuwa wa kwanza kuweka picha iliyomuonesha Nay ‘akibusiana’ na Shamsa kupitia ukurasa wake wa Instagram hivyo kuwapandisha hasira Siwema na Dick kwani alionekana kufurahishwa na ‘pea’ hiyo.
GPL
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...