2014-11-21

DIAMOND AKAMILISHA ‘TAKEU’ KWA MADEMU



Stori: Hamida Hassan
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amekamilisha ‘TAKEU’ kwa mademu baada ya kufanikiwa kutembea na mademu wanaosifika kwa uzuri kutoka Tanzania, Kenya na Uganda.

Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Historia inaonesha dogo huyo kutoka Tandale aliwahi kufanya kazi na msanii mrembo kutoka nchini Kenya, Avril na ikadaiwa licha ya kukutana kikazi jamaa alimsaliti mpenzi wake wa enzi hizo, Penniel Mwingilwa.

Beautiful Onyinye, Wema Sepetu.

Aidha, Diamond amekuwa mpenzi wa Beautiful Onyinye, Wema Sepetu kwa muda mrefu kabla ya hivi karibuni wawili hao kuamua kupeana likizo.

Mdada anayetisha kwa uzuri na mkwanja nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’.

Katika kukamilisha TAKEU ambayo ni staili ya muziki ya Msanii Nice Lucas ‘Mr Nice’ inayogusa nchi hizo za Afrika Mashariki, Diamond juzikati alimnasa mdada anayetisha kwa uzuri na mkwanja nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ na kufanya naye project ambapo inadaiwa wawili hao walivuka mipaka na kupeana penzi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...