2014-12-17

ANUSURIKA KUUAWA KATIKA WIZI WA PIKIPIKI MAGOMENI, DAR

Mtuhumiwa akiwa katika hali mbaya.



KIJANA ambaye jina lake haikufahamika mara moja, amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za wizi wa pikipiki jijini Dar.Tukio hilo la kusisimua limetokea asubuhi ya leo Magomeni-Mwembechai, ambapo lilisababisha foleni ndefu ya magari wakati kijana huyo akiadhibiwa na wananchi.

Damu ikiwa imetapakaa eneo ‘alilosulubiwa’ mtuhumiwa. Mtuhumiwa wa wizi akiwa amechakazwa kwa kipigo.

Mashuhuda wa tukio hili walisema kijana huyo na wenzake waliiba pikipiki mbali na hapo Mwembechai ila katika purukushani na wamiliki wa chombo kile, kijana yule alijikuta akianguka kutoka kwenye pikipiki eneo lile na kuzingirwa na waendesha pikipiki wa pale wanaojulikana kama ‘bodaboda

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...