Kwenye pesa mara nyingi uaminifu huwa unakuwa na nafasi ndogo sana, hata ukiangalia comment za watu kwenye story hii utajua tu uaminifu una nafasi gani kwenye pesa.
Jamaa mmoja Peter Angelina ambaye ana taaluma ya udaktari lakini kutokana na kiwango chake cha elimu kutomruhusu kufanya kazi Uingereza, aliona aendelee kutafuta riziki kupitia biashara ya kuuza tissue pamoja na vitu vingine vidogo vidogo katika mitaa ya Uingereza ambapo kwa hapa Tz wanafahamika kama Machinga.
Peter aliiona briefcase ikianguka kutoka juu ya taxi, akaifuata na kugundua kuwa ndani kulikuwa na pesa kiasi cha Paundi 16,000 ambazo ni zaidi ya mil.40 za Tz, akazipeleka kituo cha Polisi ili wamtafute muhusika wampatie.
Baada ya muhusika kufika kituoni hapo kwa ajili ya kuchukua briefcase yake ambayo mbali na kiasi hicho cha pesa kulikuwa na simu ya mkononi pia, mwenye briefcase hiyo alimpatia Peter kiasi cha pesa ambacho ni sawa na laki mbili na nusu za Tz.
Alichokifanya ni wengi wamemponda eti kajifanya muaminifu mbele ya pesa? Nitafurahi kusikia chochote kutoka kwako, wewe unasemaje?
0 comments:
Post a Comment