Ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond'.
LILE ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kumchefua mrembo huyo kiasi cha kulisusa.
Tukio hilo lilijidhihirisha wazi mbele ya paparazi wetu juzikati nyumbani kwa staa huyo, Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka hadharani kuwa kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo alilozawadiwa na Diamond kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.
“Bwana acha nitumie hili gari lingine kwenda airport hilo Murano sitaki hata kulisikia, sijui najisikiaje hata nikiliona,”alisikika Wema.
Paparazi wetu baada ya kusikia Wema akionesha wazi kuwa analichukia gari hilo, alimuuliza sababu inayomfanya alichukie ambapo alisema hajui ni kwa nini analichukia ingawa ni mali yake.
0 comments:
Post a Comment