Polisi mkoani Tanga wamesema wataendesha msako wa kuwakamata watu wanaofanya biashara ya ngono katika nyumba za starehe na mitaa maarufu kwa biashara hiyo.
Msako huo unatokana na malalamiko ya muda mrefu ya wakazi wa Jiji la Tanga hususan wanaoishi mitaa ya Centrol na Ngamiani ambako biashara hiyo inadaiwa kukithiri.
Akizungumza na Mwandishi hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Freisser Kashai alisema wamepokea malalamiko hayo muda mrefu, walishindwa kuchukua hatua mara moja kwa kuwa walikuwa wakiyafanyia uchunguzi.

Alisema baada ya kumalizika kwa uchunguzi wao, wamejipanga kuwakamata wote wanaohusika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Kamanda huyo alisema kuendelea kuiacha ishamiri inachangia kuporomosha maadili ndani ya jamii.
Kamanda Kashai alisema cha kusikitisha, biashara hiyo sasa inafanywa mpaka na watoto wadogo wenye umri wa kwenda shule na wanafunzi wanaosoma shule za bweni ambao wengi hutoroka nyakati za usiku na kwenda kujiuza kwenye nyumba za starehe.
Alisema polisi wana taarifa zote za majengo na maeneo kunakofanyika biashara hiyo. “Operesheni yetu itaanza muda wowote kuanzia sasa, tutawakamata na kuwafikisha mahakamani,” alisema.
Akizungumzia usalama wa raia na mali zao katika sikukuu ya Mwaka Mpya, Kamanda Kashai ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutoa taarifa kwa polisi pale watakapobaini viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.
“Kila mara tumekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano na wananchi mitaani kuwaelimisha namna ya kushirikiana na Polisi kuwafichua wahalifu, hii imesaidia kupunguza matukio hayo kwa asilimia kubwa,” alisema Kashai.
0 comments:
Post a Comment