Msanii wa Kundi la East Coast Team, King Crazy GK jana amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mwanadada mrembo na mwenye sauti matata Diva Loveness Love wa Clouds Fm.
Akizungumza na kipindi cha Mkasi kupitia EATV Jumatatu (Jan.12), GK alisema Diva ni mpenzi wake na anampenda sana kuliko alivyowahi kumpenda mtu yoyote kimapenzi, huku akidai kuwa mitandao ya kijamii imechangia ku-boost penzi lao.

“inawezekana, kwa sababu ni mwema kwanza halafu na mitandao, unakuta watu wana exchange information, mpenzi wangu wa sasa anazungumziwa sana kwa sababu kuna njia nyingi za kupashana habari” alisema GK.
Baada ya kauli hiyo mwanadada Diva ambae ni mtangazaji wa Ala za Roho ndani ya Clouds Fm, kupitia ukurasa wake wa instagram aliandika: “Aww My baby .. My Gk told ya .. I love him so much .. I love his Charm and his intelligence . best Man On earth.. eeh niambieni kasemaje??”
Hii inaonyesha kuwa kweli ni wapenzi na Mapenzi yao yana nguvu kubwa. Bongo Swaggz inawatakia kila la kheri na mpendane zaidi na zaidi.
0 comments:
Post a Comment