Mimi siyo nabii, lakini leo hii napenda kutoa maono yangu juu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kuhusu ya uwezekano wa kumwagika damu kutokana na usomaji wa alama za nyakati.
Tukubali kwamba dunia ya leo inaogopa sana maono hasa yanayotishia madaraka ya wanasiasa mufilisi.
Maono ni elimu inayomhusu Mwenyezi Mungu awezaye na ajuaye yote.
Hivyo basi, mwanadamu kujidai anajua sawa na Mungu ni kufuru ya hali ya juu. Lakini Mungu huyo aliyemuumba mwanadamu kwa mfano na sura yake, anaweza kumfunulia mwanadamu mambo fulani ili aweze kuwaeleza wanadamu, kuwaonya, kuwahabarisha au kuwaelekeza.
Maovu yanavyoendelea kutokea katika nchi yetu kwa kusoma alama za nyakati, najiuliza swali moja. Je, Tanzania inakwenda kuingia katika historia ya umwagaji damu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu?” Hakika kwa maovu mengi ya nchi yetu hivi sasa ni wazi, Taifa halipo salama.
Miaka mitatu sasa nchi imepitia katika matukio na maovu ya ajabu ambayo yanashtua mustakabali wa jamii nzima.
Kumekuwa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kumekuwa na utekaji wa raia wema na kujeruhi, mfano Dk Stephen Ulimboka, marehemu Dk Sengondo Mvungi, mauaji ya David Mwangosi, na kadhalika.
Taifa na Serikali ya CCM, inaendelea kutikiswa na ufisadi wa mabilioni ya fedha za wananchi bila hatua maalumu kuchukuliwa na serikali iliyoko madarakani chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Uvunjaji wa haki za binadamu umeendelea kutokea mara kwa mara. Usalama wa raia umetikiswa mara nyingi sana na leo tunashuhudhia ‘Panya Road’ wakihatarisha maisha ya raia jijini Dar es Salaam bila Jeshi la Polisi kuwa na uhakika, Panya Road ni nani hasa?
Utekaji, ukandamizaji wa vyama vya upinzani, kujeruhi na hata kuua wanachama wao katika mikutano umeendelea kutokea na Serikali kushindwa kuchukua hatua kwa wauaji hao.
Udini umeingizwa katika siasa na umewagawa waumini wa madhehebu mbalimbali kwa kupandikiza chuki na wanasiasa hata kusababisha mauaji ya viongozi wa dini. Kulipua Parokia ya Olasiti Arusha mbele ya Mwakilishi wa Baba Mtakatifu na kusababisha vifo vya watu kufa na makumi kadhaa kujeruhiwa ni alama mbaya ya kuelekea umwagaji damu kati
0 comments:
Post a Comment