Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini Ali Makame akitoa salaam za ufunguzi wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye vya Skuli ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wananchi wakifurahia mkutano wa Kinana.
Mbunge wa Viti Maluum Kidawa Hamisi akitoa hotuba na elimu kwa waliohudhuria mkutano kwenye viwanja vya Skuli, Nungwi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nungwi wilaya ya Kaskazini A kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja Skuli.
Wananchi wa Nungwi wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa akihutubia ambapo alisisitiza wananchi hao kushikamana kwenye maswala muhimu ya kimaendeleo na kuwapuuza wanaotaka kukwamisha maendeleo.
Bango la kumkaribisha Kinana Nungwi likiwa na ujumbe wa kumpa hongera kwa kusimamia vyema ilani ya Chama.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akihutubia wakazi wa Nungwi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakihutubia wananchi wa Nungwi wilaya Kaskazini A ambapo aliwaambia viongozi wa CCM kutenda haki kwani ndio wataheshimika kwa wananchi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Nungwi na kutoa pongezi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha utiaji saini wa makubaliano ya kuungana kwa chama cha SPLM kutoka Sudani Kusini yaliyofanyika Arusha tarehe 21 Januari na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi mbali mbali.
Wanachama wapya wa CCM Nungwi wakionesha kadi zao wakati wa kuapishwa.
Vijimambo
0 comments:
Post a Comment