Msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ akipozi.
BAADA ya hivi karibuni kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, Maximilian Bushoke, msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kwamba hahitaji tena mwanaume kwa sasa.
BAADA ya hivi karibuni kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, Maximilian Bushoke, msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kwamba hahitaji tena mwanaume kwa sasa.
Akipiga stori na paparazi wetu, Jini Kabula alisema kutokana na kwamba alikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi muda mrefu na Bushoke na hakuona faida yoyote, anaujutia muda wake na sasa ameamua kuachana na masuala ya mapenzi na amejikita kwenye kazi zaidi.
“Nimegundua kwamba wanaume ni watu wanaonipotezea muda tu maana nilimsubiri Bushoke muda wote huo lakini alivyokuja Bongo akanipotezea hivyo nimeamua kujikita kwenye kazi zaidi,” alisema Jini Kabula.
0 comments:
Post a Comment