Mwigizaji na mwongozaji wa filamu hapa bongo, Jacob stephen ‘JB’ ambae pia ni mkurugenzi na mliliki wa kampuni ya maswala ya filamu ya Jerusalem alitupia picha hiyo hapo juu na kuibandikia maelezo haya;
“Mzee huyo mwenye kofia anaitwa Chimbeni herry, hii ni moja kati ya scene utakazo ziona ndani ya mzee wa swaga.Hapo ni zanzibar,kati ya wasanii wazuri ambao hawajatumika vizuri ni pamoja na huyu.
Jamani anaweza,mwaka huu nitacheza filamu mbili (2) tu, lakini nitaanda nyingi ambazo nitawaachia watu wengine waonekane hasa Zanzibar,Mwanza,Arusha,Dodoma na Mbeya.
Hakika tutazalisha mastaa wengi kama tulivyofanya kwenye bado natafuta,wageni wangu na Chausiku,Jerusalem ni yenu vijana”. JB alimaliza
0 comments:
Post a Comment