Dar es Salaam. Idadi ya wajawazito wanaojifungua kwa njia ya upasuaji nchini imeongezeka kwa asilimia 31 katika kipindi cha miaka 11.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa alisema hayo jana katika kongamano
lililohusu magonjwa ya wanawake.
Alisema takwimu hizo zinaonyesha kuwa mwaka 2000
waliojifungua kwa njia hiyo walikuwa ni asilimia 19, lakini ilipofika
mwaka 2011 walifikia asilimia 50.
Alisema tafiti zinatakiwa kufanyika ili kubaini chanzo.
Mtawa alisema licha ya kwamba kujifungua kwa
upasuaji ni njia ya kuokoa maisha, lakini utaratibu huo unaonekana ni
hatari kwa wajawazito.
Mkunga katika hospitali hiyo, Gloria Mkusa alisema kwa mwaka huzalisha wanawake wengi kwa upasuaji kuliko njia ya kawaida.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Sebalda Leshabari aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa upasuaji siyo njia salama.
0 comments:
Post a Comment