Kiongozi wa mashtaka nchini Argentina Alberto Nisman amepatikana amefariki nyumbani kwake baada ya kumshtumu rais wa taifa hilo
Kiongozi maarufu wa mashtaka nchini Argentine amepatikana amefariki ndani ya nyumba yake mjini Buenos Aires, baada ya kumshutumu Rais Cristina Fernandez kwa kuzuia uchunguzi wa mashambulio mabaya zaidi ya ugaidi kuwahi kufanyika nchini humo.
Alberto Nisman alikuwa amepangiwa kutoa maelezo ya kina kwa bunge la taifa hilo.
Alikuwa akisimamia uchunguzi kuhusiana na mlipuko katika kituo kimoja cha kijamii kilichokuwa kikisimamiwa na wayahudi mjini Buenos miaka 20 iliyopita ambapo watu watano waliuwawa.
&nbs
Juma lililopita bwana Nisman alimshutumu Rais Fernandez na wakuu wengine kwa kuzuia uchunguzi huo.
0 comments:
Post a Comment