Janeth Mlahagwa (18) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi “Albino”, mkazi wa Kijiji cha Mtumbatu, Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro ambaye anadai kwamba kifo kilimsonga kutokana na hali yake kuwa mbaya kila kukicha kwa kukosa matibabu na badala yake alikua akipewa vidonge vya kupunguza maumivu.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni katika hospitali binafsi ya upasuaji wa mifupa na viungo cha Burere, wilayani Kibaha kwa Mathias, Mkoa wa Pwani, Janeth alisema kwamba kutokana na umaskini wa wazazi wake ambao ni wakulima wa jembe la mkono alinazimika kupewa vidonge vya kutuliza maumivu ambavyo havijamsaidia.
Janeth ambaye amefuatana na mzazi wake katika hospitali hiyi ni mtoto wa kwanza kati ya watoto sita katika familia yao na watatu kati ya hao ni Albino.
ALIVYOKUTWA KIJIJINI
Akieleza zaidi alikuwa na haya ya kusema:
“ Namshukuru Mungu aliyempeleka Mkurugenzi wa Hospitali ya Berere, Dk. Joseph Theodore Bake ambaye alitembelea kijijini kwetu na kunikuta nikiwa katika hali mbaya naakanichukua kuja kunitibu hapa na ugonjwa umeshajulikana baada ya vipimo.

UVIMBE UNAOMTESA
“Mateso ninayoyapata leo hii ni kwa sababu ya uvimbe katika shavu, ulianza kama kipele Julai, mwaka jana, baadaye kipele hicho kikaanza kuvimba.
“Mama akawa ananipeleka katika zahanati mbalimbali lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwani nilikuwa napewa dawa za kutuliza maumivu tu ambavyo havikunisaidia kunitibu.
UKATA ULIFANYA NISIPATE TIBA
“Mama akawa ananipeleka katika zahanati mbalimbali lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwani nilikuwa napewa dawa za kutuliza maumivu tu ambavyo havikunisaidia kunitibu.
UKATA ULIFANYA NISIPATE TIBA
“Bahati mbaya, ukata katika familia ulichangia mimi kuwa na hali mbaya kwani wazazi wangu hawakuwa na la kufanya kwa sababu hawakua na fedha za kunipeleka hospitali kubwa.“Baadaye wakawa wanajitokeza waganga wa kienyeji kuja kunitibia lakini familia ilikataa kwani wengi wao wanakua na nia mbaya, nilibakia kulia na kumuomba Mungu.
MUNGU ASIKIA MAOMBI
MUNGU ASIKIA MAOMBI
“Mungu alinisikia maombi yangu akawa amejitokeza Dk. Bake aliyekuja kijijini kwetu akaniona nimelala nje ya nyumba yetu huku nikilia kutokana na maumivu makali, alisimamisha gari lake na kuja kwangu kuniangalia.
“Baada ya kuniona aliwaita wazazi wangu na kuwaambia waniandae na kuja huku Kibaha. Alituchukua katika gari lake na kuja nasi hadi hapa Kibaha katika hospitali ya Bake.
“Baada ya kuniona aliwaita wazazi wangu na kuwaambia waniandae na kuja huku Kibaha. Alituchukua katika gari lake na kuja nasi hadi hapa Kibaha katika hospitali ya Bake.
“Alitugharamia kitu kitu, nilifarijika sana kuona kuwa nathaminika na mtu msomi kama huyu kwani pale kijijini baadhi ya watu waliniona kama siyo binadamu, kuumwa kwangu kulikuwa hakuwasikitishi.
MATOKEO YA UCHUNGUZI
“Baada ya kufika hapa Kibaha siku iliyofuata nilifanyiwa uchunguzi na Dk. Bake na kuona ugonjwa unaonisumbua ni dalili ya kansa, ili kuhakikisha alichukua kipande cha nyama katika shavu akapeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili na kudhihirika wazi kwamba ni kansa.“Niliambiwa matibabu yake ni katika Hospitali ya Ocean Road ambapo ameniahidi kunipeleka huko kutibiwa.
“Nasikitika kwa sababu shule sijasoma, nimekua nkiiishi kwa hofu hasa ninaposikia kwamba maalibino wenzangu wamekua wakiuawa hovyo, sitembei mbali na nyumbani kwa hofu ya kukamatwa.
“Namshukuru sana Dk. Bake ambaye amenionea huruma kuliko hata serikali na tunaishi na mzazi wangu hapa kwa gharama yake, Mungu ambariki”alisema Janeth huku akitokwa na machozi

DAKTARI ANENA
Dk. Bake naye amesema kwamba ameamua kumsaidia mtoto huyo kutokana na hali aliyonayo na alikua akiishi na ugonjwa kwa kusubiri kifo.
“Huyu ni binadamu kama wengine kiasi kwamba anapolia na kukata tamaa juu ya maisha yake inasikitisha wakati sisi tupo, nilijisikia vibaya alipokua akilia bila msaada, niliamua nimchukue, ili kumtoa hofu niliwachukua na wazazi wake.

Nitajitahidi kumtibu huko Ocean Road na gharama zote nitazisimamia”alisema Dk Bake ambaye ni bingwa wa upasuaji wa mifupa na viungo.
0 comments:
Post a Comment