2015-01-05

ISHAALAA;SHEREHE ZA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.A.W.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) wakati alipojumuika na Mashekhe, Viongozi na Waislamu mbali mbali katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W 
yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,(pichani) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akitia ubani kama ishara ya Ufunguzi wa Maulid hayo,[Picha na Ikulu.] Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakia Bilali (katikati) akiwa na Wake wa makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) na Mama Pili balozi Seif (kulia) pamoja na Wake wa Viongozi mbali mbali na wananchi wa kawaida 
wakijumuika katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita,[Picha na Ikulu.]Akina Mama kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiwa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja palipofanyika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W
 
 ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Kadhi Mkuu wa zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary akifuataiwa na makamo wa Pili wa Rais Alhaj Seif Ali Iddi wakisimaMa kwa pamoja na waislamu wengine 
na Viongozi wakati wa Kumswalia Bwana Mtume 
Muhammad S.A.W.katika sherehe ya Maulid iliyofanyika jana viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali vya Quran na Waislamu mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya 
kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad S.A.W zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja kama wanavyoonekanwa Pichani,[Picha na Ikulu.]Wanafunzi wa Madrasatul Dhuriyatul Islamia kutoka Kisiwani Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]Ustadh salum Rashid kutoka Amani Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Mlango wa Barzanji(4) wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...