Katibu wa Kamati ya Tathmini wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Ernest Mwamwaja (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kampuni zinazowajibika kwa jamii kutambuliwa Machi mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii, Abraham Shempemba na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Dickson Hyera.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI mbali mbali zinazotoa huduma kwa jamii zinatarajiwa kutambuliwa na kutolewa tathimini ya uwajibikaji wake machi mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Ushauri wa Biashara, Dickson Hyera alisema lengo ni kurudisha sehemu ya biashara kwa jamii kama sehemu ya shukrani.
Alisema pia italeta faida nyingine ikiwa ni pamoja na kuleta mahusiano mazuri na kampuni nyingine ambapo matoko yatakayotoka yataleta hamasa kwa kampuni nyingine kurudisha sehemu yao ya biashara katika jamii.
Hyera alisema tafiti zinaonesha kuwa kampuni za nje ndo zinahusika zaidi katika jamii hususani katika masuala ya elimu, mindombinu, maji na huduma nyingine za kijamii.
"Tayari kunataasisi nyingine zimeshafanya marejesho hayo na nyingine hazijaleta hivyo nyingine zijitokeze kuonesha nia ya kushiriki ili ziweze kunufaisha jamii," alisema.
Aliongeza kuwa mchakato huo pia unalenga kutathimini kwa kulinganisha takwimu za mirejesho ambayo inafanywa na taasisi kuthaminisha na kung'amua kuhusu manufaa hayo na gharama zake.
Alisema madhumuni makubwa ya tathmini hiyo yanajumuisha kuona jinsi gani taasisi mbalimbali zinazojitoa kwaajili ya kusaidia jamii, kutambua na kuthamini wanaofanya vizuri, jinsi taasisi hizo zinavyochangia kufanya maisha ya wanajamii kuwa bora kwa kuzingatia idadi ya misaada ambayo inatolewa na thamani zake.
Naye Katibu wa Kamati ya Tathmini Ernest Mamwaja alisema kuna watu wananufaika lakini hawajui wamesaidiwa na nani hivyo watajua, pia wanaotoa msaada wanaweza kuleta nguvu katika maeneo ambayo manufaa yake ni makubwa.
Alisema tafiti ambazo zimeonesha kuwa kampuni ambazo zinarejesha kwa jamii zinamanufaa makubwa ikiwa ni pamoja na soko kupanda, hivyo lengo si kuangalia nani mshindi au nani amefanyanini ali ni kwaajili ya manufaa ya watanzania.
0 comments:
Post a Comment