Kupitia ukurasa wake wa kwenye mtandao wa INSTAGARM, Wolper alifunguka;
“Habari Followers pamoja na wa Tanzania wote ambao naamini huwa mnaingia katika page yangu ya insta.Nimepokea zawadi hii ya Coca cola kwa siku 6 .
Na sio kwamba sikutaka kupiga picha kama wenzangu au ku post kama wenzangu, nilikuwa natafakari kweli kampuni kubwa ya kitaifa na kimataifa inaweza kutumia gharama kubwa kuandika majina yetu bila kuchukuwa hata nafasi na heshima kubwa tuliyonayo kutushirikisha tu katika makubaliano ya kuandika majina yetu katika makopo yao.
Maana naamini mafan's wa Wolper wangeweza kushare na Coca cola kutokana Jina Langu kuwa label katika makopo yao.
Sasa Naamini tuna wanaharakati,wabunge,wanaSheria pamoja na serikali ambao huwa wanafwatilia wale wauza CD wa kariakoo basi Naomba Juhudi hizi mzihamishie huku katika kampuni hii kubwa ya kimataifa Coca cola ili kutetea haki za wasanii na sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki jamani.
Sijui kama wasanii wenzangu walilipwa siwezi kuwasemea lakini haya ni mawazo yangu binafsi”. Wolper aliishia hapo.
0 comments:
Post a Comment