2015-02-02

‘AIRTEL YATOSHA ZAIDI’ YAZINDULIWA, WATEJA KUONDOKA NA

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Levi Nyakundi (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano (kulia) akitoa ufafanuzi wa huduma mpya ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’.

Aina ya magari yatakayotolewa.
Nyakundi na Singano wakizindua moja ya magari yatakayotolewa kwa wateja wa Airtel.
Moja ya magari yatakayoshindaniwa.
Nyakundi na Singano wakiwa na bango lenye nembo ya Airtel Yatosha Zaidi.

Sehemu ya waandishi wa habari waliofika kwenye tukio hilo.

KAMPUNI ya mtandao wa simu ya Airtel imezindua huduma mpya ya vifurushi vya muda wa maongezi, mtandao na meseji unaokwenda kwa jina la ‘Airtel Yatosha Zaidi’. Huduma hii ina unafuu zaidi ya huduma ya mwanzo iliyotambulika kama ‘Airtel Yatosha’.

Wakizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Mlimani City, Dar, Mkurugenzi wa Masoko Levi Nyakundi na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano, wa Airtel, walisema wateja wao watazawadiwa gari aina ya Toyota IST itakayotolewa kila siku kwa mshindi atakayepatikana baada ya droo ya huduma hiyo kuchezeshwa.

Wakifafanua zaidi kuhusu zawadi hiyo, wakurugenzi hao walisema kwa kupiga *149*99# kununua Airtel Money au kwa kununua vocha za Airtel Yatosha zilizopo kwenye maduka yote nchini, mteja wa Airtel anaweza kujiunga na vifurushi vya ‘Yatosha Zaidi’ na kuweza kuingia katika droo itakayomwezesha kushinda gari hilo. (HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL)

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...