2015-02-02

Rais Kikwete ammwagia sifa kibao Diamond PlatinumzIKIWEMO NA

 At Mwalimu Nyerere Airport with my manager,Babu tale
Dar es Salaam. Mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’ jana aliziteka nyoyo za wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maadhimisho ya miaka 38 ya kuanzishwa kwa chama hicho yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.


Pamoja na wasanii wengi walioalikwa kutumbuiza katika sherehe hizo, Diamond alitajwa zaidi na viongozi wa chama hicho tawala wakiongozwa na Mwenyekiti Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete aliyesema kuwa sifa za mwanamuziki huyo zimefika mpaka nje ya Afrika Mashariki.


“Juzi nilikuwa Ethiopia na katika duka moja nilimkuta msichana akisikiliza na kucheza wimbo wa ‘My number one’. Nilimuuliza unauelewa wimbo huo, akanijibu hapa, lakini naupenda. Nilimwambia kuwa huo ni wa msanii mkubwa kutoka Tanzania…ni maarufu nyumbani, Afrika na duniani pia,” alisema Rais Kikwete.


Akijua kuwa wapo wapenzi wengi wa msanii huyo waliokuja kumwona akipanda jukwaani, Rais alisema kuwa anaifupisha hotuba yake ili msanii huyo atoe burudani na kukata kiu ya wanachama na wafuasi wa CCM.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...