Ali Kiba jukwaani Sauti za Busara 2015.
Katika shoo hiyo Ali Kiba alipanda jukwaani majira ya saa sita usiku na kuendelea kwa zaidi ya masaa mawili, alikonga nyoyo umati wa mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo huku akishangiliwa wakati wote na mashabiki wake waliojaa uwanjani hapo.
Onyesho hilo Ali Kiba alilitawala jukwaa kwa kuimba muziki wa ‘live’ bila kutumiaa play back, hali aliyoitendea haki na umati wa watu waliofurika kumkubali zaidi hasa alipotoaa zawadi ya kipekee kwa kupiga nyimbo zaidi ya 12.
Katika kunogesha shoo hiyo, mdogo wa Ali Kiba, Abdu Kiba naye alionyesha umahiri wake kwa kupanda jukwaani huku wakiwateka kwa wimbo wa ‘Usha wahi kupendwa’ ambapo wawili hao waliutendea haaki kwa kukatika mauno na aina ya uchezaji wake.
Licha ya ugumu wa kuimba ‘live’ kwa wasanii wengi hapa Nchini, Ali Kiba aliweza kuwachezesha mashabiki ikiwemo kwenda nao kwa stepu mbalimbali za uchezaji pamoja na kuimba nao. Katika nyimbo hizo zaidi ya 12, Ali Kiba aliweza kuimba nyimbo kadhaa ikiwemo kuchanganya baadhi ya nyimbo zake, pamoja na nyimbo zingine ikiwemo alizoshirikishwa na wasanii wengine huku mwisho akimaalizia na kibaao cha ‘Mwana Dar es Salaam’.
Katika kile kinachoonyesha kukubalika, fans mbalimbali wakiwemo raia wa kigeni na wa kutoka mataifa mbalimbali walimkubali Ali Kiba huku kila mmoja akitaka kupiga naye picha ya kumbukumbu hasa kutokana na shoo hiyo ambayo wengi waliikubali kwa mikono miwili.
Jackie Julius wa mo dewji (mwenye chui chui) akifuatilia na kurekodi moja kwa moja shoo hiyo.
Voko list wakimuongoza Ali Kiba kwenye shoo hiyo.
0 comments:
Post a Comment