Baada ya maswali kuwa mengi kuhusu uhusiano baina ya mtangazaji wa EATV/EA Radio, Sam Misago na mwimbaji Mwasiti Almasi, wawili hao wameamua kuzikanusha kwa pamoja taarifa hizo kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV jana Feb 6.
Tarehe 6 Feb. ilikuwa ni birthday ya Sam Misago, na katika kuisheherekea aliwakaribisha studio za EATV wasanii Mwasiti, Damian Soul na Makomando kusheherekea naye mbele ya watazamaji wa kipindi hicho.
Licha ya kuwa Mwasiti alikuwa ameshakanusha siku kadhaa zilizopita, lakini wawili hao walitumia fursa hiyo wakiwa pamoja kwenye kipindi kukanusha kuwa wao sio wapenzi bali ni marafiki wa takribani miaka sita sasa.
Baada ya zoezi la kukata keki na kulishana kukamilika, Sam alimkaribisha Chitty kuweka sawa taarifa za uhusiano wao. Sam: “Labda Mwasiti anaweza akazungumza na watu akawaambia watu what is going on.”
“Naomba niwaambie watu kwamba mimi na Samweli, we are just friends tumekuwa marafiki kwa muda mrefu sana kwa miaka sita, mi namjua Sam sio vile ambavyo watu wanataka nimjue Sam, mi namjua Sam kivingine, lakini watu wametengeneza mazingira ya kama mpenzi”alisema Mwasiti.
Mwasiti pia alitumia nafasi hiyo kuahidi kumuweka wazi mpenzi wake ifikapo mwezi March mwaka huu.
“Mwasiti napromise March ntamweka boyfriend wangu kwenye mtandao, nawaomba kina dada kule msijali mchukueni tu Samweli sio wangu.” Alimaliza
GPL
0 comments:
Post a Comment