2015-02-09

Mama mzazi wa Nay wa Mitego anahisi mwanae ni----------- na hataki kupokea fedha yake


Mama mzazi wa Nay wa Mitego anahisi mwanae ni mfuasi wa jamii ya siri ya freemason na ameanza kusita kupokea fedha kutoka kwake.


Kwa mujibu wa mama yake, mafanikio ya haraka ya Nay yakiwemo kujenga nyumba ya kifahari, kumiliki magari kadhaa na maisha yake ya kimilionea, vimemfanya aamini maneno yanayosemwa na watu au kuandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa mwanae amepata utajiri huo kwa njia isiyo halali.

“Kuna kipindi ambapo nimetoa wimbo wa Mr Nay baada ya kutoka ile video nakumbuka mimi mama yangu huwa nampelekeaga hela ya matumizi kila baada ya wiki mbili au mwezi mmoja. Kuna kipindi nilimpelekea hela akasema ‘no’ mbona mimi hela bado ninayo,” Nay alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.

Nay anasema alimpelekea mama yake kiasi cha shilingi laki mbili ama tatu na akagundua kuwa mama yake hasemi ukweli na kuna kitu kilikuwa kikimsumbua akilini.

“Baada ya hapo akaniambia ‘kuna habari nasikia kuhusu huu wimbo wako huu nimeona mambo ya ajabu ajabu mule nimeona magazeti majirani wamekuja wameniambia hivi na hivi’,” aliongeza Nay.

“Halafu bahati nzuri nilikuwa nimetoka kununua hii gari yangu ambayo natembelea sasa hivi ‘Morano’ alivyoniuliza hivyo nikaona mama yangu hataki hela yangu sababu ana wasiwasi na hiki ambacho watu wanaongea. Hilo ni tatizo lililonipa wasiwasi na moyo wangu ukaingia unyonge, for real kabisa nikawa mpole.

“Lakini nikawa na imani kwamba endapo mama yangu angekuwa anatambua kwamba huu muziki ungekuja kuniweka sehemu uflani tangu zamani angekuwa ananisupport zile hustle mazingira magumu niliyokuwa napitia angekuwa anajua basi sasa hivi ningekuwa naenda naye sawa.”

Nay amesisitiza kuwa mali anazopata ni neema za Mungu tu.

“Mwenyezi Mungu tu ameamua kuninyooshea kuniwekea mambo yangu sawa japokuwa bado sijafika pale ninapotaka kufika,” alisisitiza rapper huyo.
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...