MBUNGE wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeish Hilaly amesema hatajiuzulu ng’o nafasi yake kama Mbunge kwa sababu za CCM kushindwa vibaya katika uchaguzi wa marudio uliofanyika juzi katika kata tatu na mitaa miwili wilaya ya Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa.
Uchaguzi huo uliofanyika katika kata za Msua ,Kizwite na Chanji pamoja na mitaa miwili ya Bangwe kata ya Izia na Tambazi kata ya Sumbawanga mjini, ulikuwa wa marudio baada ya kuahirishwa kufanyika Desemba 14 , mwaka jana.
Uchaguzi uliokuwa ufanyike Desemba 14 mwaka jana , katika kata hizo uliahirishwa kutokana na kasoro mbalimbali na kusababisha aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake ufanyike.
Alisema licha ya CCM kufanya vibaya katika uchaguzi wa marudio bado CCM ina matumaini na nafasi kubwa ya kushinda kwa nafasi za udiwani , ubunge na urais katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment