Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakitashiriki uzinduzi wa zoezi la kampeni ya uhamasishaji wananchi kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura unaotarajiwa kufanywa Jumatatu ijayo na Waziri mkuu Mizengo Pinda katika mji wa Makambako mkoani Njombe.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema hatua hiyo inachukuliwa kwa kile alichokiita kuwa ni ubabaishaji unaofanywa na Tume ya Uchaguzi nchini wa kuendesha zoezi hilo kinyume cha sheria na mfumo wa uandikishaji wapiga kura kwa Teknolojia ya Biometric Voter Registration, BVR.
Mbowe ambaye ni kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni amesema ili mfumo wa BVR utumike vizuri na raia kujiandikisha na kupiga kura kwa haki, maandalizi ya zoezi hilo yalipaswa kufanyika kwa kipindi kisichopunguaa mwaka mmoja.
Amesema ukimya wa muda mrefu wa Tume ya uchaguzi juu ya lini zoezi hilo limepangwa kufanyika umevitia shaka vyama vya siasa na hasa CHADEMA ambayo kwa kutumia mbinu binafsi imefanikiwa kupata nyaraka za tume ilizoandikiwa na mtaalamu wa teknolojia hiyo kuwa kwa muda uliosalia watanzania hawawezi kuandikishwa na kupiga kura kwa mfumo wa BVR.
Hata hivyo Mbowe amesema vikosi vya vijana hao vitafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Ametoa tamko hilo alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Uongozi wa chama hicho kwa mikoa mitano inayounda kanda ya nyanda za juu kusini kikao ambacho kilitanguliwa na uzinduzi wa uundwaji wa mafunzo ya awali ya ulinzi na usalama wa CHADEMA unaojulikaana kwa kifupi kama FTP.
Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare amesema kikosi hicho cha vijana 360 kitatumika kama wakufunzi wa vijana 200 kutoka katika kila kata ya mikoa ya kanda hiyo ili vijana hao wakitambue chama chao na kukisaidia kwenye uchaguzi mkuu ujao.
0 comments:
Post a Comment