Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kusogeza mbele zoezi la kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba inayopendekezwa ili uandikishaji wananchi katika daftari la wapiga kura ufanyike kwa weledi
Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Ubungo John Mnyika amesema kwa mujibu wa Katiba ni lazima wananchi wajiandikishe kwanza kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kupiga kura ya maoni ya Katiba pendekezwa.
Mnyika amesema muda uliowekwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura hautoshi.
Akizungumzia mchakato wa uandikishaji daftari la wapiga kura kwa kutumia vifaa vya kielektroniki vya Biometric Voters Registration BVR amesema tume ya uchaguzi inapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa jamii juu ya zoezi hilo.
Amesema CHADEMA ina mpango wa kuzindua operesheni inayojulikana kama R to R BVR kwa lengo la kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
0 comments:
Post a Comment