2015-02-19

DAAAAAA MUME WA MTU ALIVYOAIBIKA BOFYA UJIONEE MANA NI BALAAAAAA



AIBU! Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Joseph amejikuta akiaibika vikali kufuatia kudaiwa kunaswa akiwa na mwanamke mwingine ilhali yeye ni mume wa mwanamke aitwaye Sophia, Amani limenyetishiwa.

Joseph akipewa kichapo na wananchi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, aibu hiyo ilimkuta Joseph, Februari 14, mwaka huu (Siku ya Wapendanao Duniani) kwenye Kitongoji cha Nyihongo wilayani Kahama, Shinyanga wakati wadau mbalimbali walikuwa kila mtu na wake.

Mashuhuda waliliambia Amani kwamba, Joseph ni fundi ujenzi na siku ya tukio alinaswa kwenye nyumba inayojengwa na yeye lakini ikiwa bado kumalizika.“Jamaa mwenye mke alishajua kuwa Jose anamlia mali zake lakini akavumilia sana. Hakutaka kumuuliza Jose wala mke wake, yeye alitaka amfumanie laivu mwenyewe,” alisema shuhuda.



...Wakizidi kumpa kichapo.

“Sasa siku ya tukio, Jose alionwa na mtu mmoja akiingia kwenye nyumba inayojengwa. Yule mtu alishajua Jose anachepuka na yule mke wa jamaa, akaenda kumwambia ndiyo wakamzukia na kumnasa,” kilisema chanzo.

Chanzo kikaendelea kuweka wazi kuwa, baada ya Jose kunaswa alitembezewa kichapo kizito na kupelekwa kwenye ofisi za serikali ya mtaa ambapo Jose alipigwa faini ya shilingi laki tatu.
“Lakini kilichotokea sasa ni kwamba, baada ya kulipa faini hiyo, mke wa Jose naye kwa hasira aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kwao.



Mke wa aliyefumaniwa. “Alisema amelazimika kuondoka kwa Jose kwa sababu kitendo alichokifanya kimemtia aibu kubwa. Kwamba haiwezekani yeye atulie nyumbani Siku ya Wapendanao halafu mumewe akachepuke mitaani na mwanamke mwingine,” kilisema chanzo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...