SIKU chache baada ya kuibuka utata mkubwa juu ya kichanga cha kike cha mwimba Injili maarufu Bongo, Flora Mbasha huku mitandao ya kijamii ikieleza kwamba baba wa mtoto huyo si aliyekuwa mume wa mwanamuziki huyo, Emmanuel Mbasha ‘Ima’, familia ya mwanaume huyo inadaiwa kufanya kikao kizito jijini Dar ili kupata ufumbuzi, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Mwimba Injili maarufu Bongo, Flora Mbasha akiwa amejifungua kitoto kichanga Hospitalini.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia ya Mbasha, familia hiyo ilikutana Jumamosi iliyopita nyumbani kwa Ima, Tabata-Kimanga, Dar ili kulizungumza suala hilo na kuona kama wanaweza kukubaliana kukilea kichanga hicho endapo ni damu yao.
“Ndugu walitofautiana, kila mtu alikuwa na mtazamo wake hivyo wakaona bora wakutane na kutafuta jibu la pamoja kama wanalea au hawalei,” kilisema chanzo hicho.
KIKAO CHAVUNJIKA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kikao hicho hakikufikia muafaka kutokana ndugu hao kutofautiana kimisimamo kwani kila mmoja alitoa mawazo yake.
Mwimba Injili huyo, Flora Mbasha anayedaiwa kuzaa kitoto kichanga nje ya ndoa.
MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha ambaye sasa anatamba na Wimbo wa Haribu Mipango ya Shetani ambao inadaiwa amekuwa akiutumia kama kijembe kwa Flora, alisema aachwe kwanza kwani suala hilo linamuumiza kichwa na ni la kifamilia zaidi.
“Naomba mniache kwanza, sipo vizuri kwa sasa,” alisema
CLIP YAONESHA MSIMAMO
Kwa mujibu wa ‘clip’ ya sauti yake (Mbasha) aliyoituma kwa Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, yeye ana mtoto mmoja tu, Elizabeth Emanuel Mbasha ’Liz’ ambaye ana miaka kama kumi na moja.
Mbasha alisema hajui nini kinaendelea na kwamba ameambiwa habari za Flora kujifungua mtoto wa kike lakini yeye haoni kama habari hizo zinamhusu sana!
Flora Mbasha akiwa na aliyekuwa mume wake, Emmanuel Mbasha.
MSIKIE
“Mimi sijui niseme nini? Nimeambiwa kwamba Flora amejifungua. Kwa hiyo? Mbona yeye Flora hajaniambia, si anajua taarifa hizo hazinihusu? Amuogope Mungu, yeye angewaambia watu ukweli.”
Ijumaa Wikienda: “Kwa hiyo unataka kusema mtoto si wako?”
Mbasha: “Yeye anajua.”
NDUGU WA MBASHA
Ijumaa Wikienda lilizungumza na ndugu mmoja wa Mbasha (jina lipo) ambaye alizungumzia sakata la shemejiye kujifungua mtoto akiwa mbali na nyumbani:
“Haiwezi kukubalika. Yeye kama alijua amegombana na Mbasha halafu ana mimba, anangejinyenyekeza akatulia mpaka azae.
Mchungaji wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima akiwa kazini.
KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mara baada ya ugomvi wao na kuondoka nyumbani miezi saba iliyopita, Flora aliwahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari akikiri kuwa na ujauzito na kusema: “Ndiyo nina mimba lakini siyo ya Gwajima.”
AZUNGUMZIA UNDUGU WAKE NA GWAJIMA
Hata hivyo, hivi karibuni, Flora alikazia tena maneno yake kwa kusema kuwa Mchungaji wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ni anko (mjomba) wake kwa hiyo watu wajaribu kuliangalia hilo, hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mjomba‘ake.
KUHUSU MADAI KUWA MTOTO NI WA GWAJIMA
Mwanasheria: “Kwanza nataka kusema kwamba, chombo chochote cha habari ambacho kiliandika habari ya kumchafua Flora tutakishitaki. Iwe ni magazeti iwe ni mitandao ya kijamii. Wanaosema ni mtoto wa Gwajima ndiyo wanaomchafua Flora kwa sababu si kweli.”
0 comments:
Post a Comment