2015-02-23

Gardner Akanusha Uvumi wa Kuachana Mkewe Jack Pentezel..................fuatilia alichokisema hapa

Gardner Dibibi ambae ni mume wa mwigizaji wa filamu Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ amekanusha taarifa zilizoenea mtandao na kwenye magazeti ya udaku kuwa ameachana mke wake Jack.

Gardner ameimbia Bongomovies.com kuwa taarifa za yeye kuacha na mkwe wake sio za kweli japo kuwa ni kweli walikuwa natofauti za kawaida na wameshazimaliza na pia amekanusha kuwa hakumpa talaka kama ilivyoripotiwa .

“Taarifa hizo sio za kweli, sisi tuko pamoja, tulikua na matatizo ya kawaida tu lakini hatujaachana na wala sijawai mpa talaka" Gadner alieleza.

Taarifa hizo zilidai kuwa wawili hawa ambao wamedumu kwenye ndoa kwa miaka miwili na nusu sasa wameachana baada ya Gardner kumpa talaka Jack huku chanzo kikitajwa kuwa ni usaliti katika mapenzi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...