2015-02-23

Ukweli Kuhusu wa Mwanamuziki Snura wa Majanga Kujifungua Mtoto wa Pili na Kumficha South Africa Huu Hapa

Alikuwa wapi? Baada ya kupotea kwa muda mrefu, staa wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi hatimaye ameibuka na kueleza sababu za ukimya wake.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum, Snura amefunguka kwamba ukimya wake ulitokana na kwenda Afrika Kusini ‘Sauz’ kushuti video ya wimbo wake wa Najidabua na siyo kweli kwamba alikuwa mkoani Mbeya kwa mwanaume.

Katika intavyu hiyo, Snura alikanusha tetesi za kuzaa mtoto wa pili na kusisitiza ana mtoto mmoja na wanaosema maneno hayo wamekosa la kusema.
Ijumaa Wikienda: Huoni kukaa kwako kimya mashabiki wamekusahau?Snura: Hawajanisahau kabisa na hilo nililithibitisha hivi karibuni kwenye shoo niliyofanya Msasani Club (Dar), ambapo walijaa tofauti na mwanzo japokuwa mwanzoni kabla ya shoo nilikuwa nawaza wamenisahau.

Walifurahi sana kwani kwa sasa nimekuja na staili tofauti ya kukata mauno ambayo inatambulika kwa jina la Mauno ya Panya Road, yaani haya ni hatari.
Ijumaa Wikienda: Kuna habari kwamba wewe na mpenzi wako DJ Hunter wa Mbeya mmeachana, hili likoje?

Snura: Unajua katika maisha yangu Hunter ndiye mwanaume wa kwanza kumuanika na sikuwahi kuanika mapenzi yangu kabisa kabla ya hapo.
 Sasa baada ya kuwa tunatupia picha mbalimbali kwenye mitandao watu walinifuata na kunieleza kwamba ninavyofanya siyo vizuri.

Nilichukua ushauri wao na kuufanyia kazi na mpenzi wangu nikamwambia, tukaacha tabia hiyo.

Hali hiyo ya kutokuweka picha ndiyo iliyozusha maneno kibao kwamba tumeachana lakini siyo kweli.

Ijumaa Wikienda: Hivi huoni kwamba Shilole amekufunika kwa sasa wakati wewe ulikuwa juu zaidi yake?

Snura: Hicho kitu hakipo na Shilole hawezi kunifunika kwani najua kwamba siku zote mbuyu hauwezi kugeuka mchicha.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...