Vurugu zililazimu Polisi kuongeza nguvu ili kudhibiti Wafungwa
Mtu mmoja ameuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea katika Gereza moja mjini Kumasi nchini Ghana wakati Wafungwa walipokuwa wakijaribu kutoroka wakati ilipotokea ajali ya moto.
Maafisa wa usalama walipambana na Wafungwa, hali iliyosabisha mfungwa mmoja kupoteza maisha Polisi wanne walijeruhiwa.
Wafungwa hao walikuwa wakijaribu kutoroka wakati walipokuwa wakihamishwa kutoka kwenye vyumba vyao wakati moto ulipotokea.
Moto huo unaelezwa kutokea baada ya kuwepo hitilafu kwenye Taa.
Polisi walilazimika kutumia gesi za kutoa machozi dhidi ya wafungwa hao ambao walikuwa wakiwarushia fimbo, mawe na viti.
0 comments:
Post a Comment