Bi harusi mmoja kaskazini mwa India, alijikuta kwenye wakati mgumu siku ya ndoa, kisa ni ugonjwa wa mume wake mtarajiwa ambao yeye hakujua kama bwana huyo anaumwa.
Haikuwa siku nzuri kwa bwana harusi, ana tatizo la ugonjwa wa kifafa na tatizo hilo likamkuta siku ya ndoa yake na bibie Indra.
Indra alifanya maamuzi hayo magumu ambapo muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na bwana Jugal Kishore, bwana huyo alianguka ghafla kutokana na kifafa na kupelekwa Hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu, tukio hilo lilimfanya Bi harusi ashikwe na hasira kutokana na mume wake huyo mtarajiwa kumficha kwamba ana tatizo la ugonjwa huo.
Indra alibadili maamuzi, akatoa ombi la kuolewa na mmoja wa wanafamilia ya bwana harusi, ambaye alikuja tu harusini kusherehekea sherehe hiyo, jamaa akaonda hii ni bahati ya mtende kwake, baada ya bwana harusi kupata nafuu alirudi na kukuta story imekuwa nyingine harusini.
Hii mfano inakutokea wewe ungeamua nini mtu wangu?
0 comments:
Post a Comment