Wasema Jimbo la Moshi Mjini lazima liondoke Chadema
Moshi. Makada wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ‘wamegongana’ kutangaza nia ya kumrithi Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema).
Ndesamburo ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi vitatu (2000-2015), amekaririwa akidai kuwa anatafakari kama bado ana sababu ya kugombea tena au kupumzika.
Makada hao ni Katibu Mwenezi wa CCM Manispaa ya Moshi, ambaye pia ni Diwani wa Kilimanjaro, Priscus Tarimo na Buni Ramole.
Tarimo alisema jana kuwa amejipima na kuona anaweza kuwatumikia wananchi wa Moshi kama CCM itampitisha kuwania nafasi hiyo.
Alisema ana uwezo wa kuzitafutia majibu changamoto zinazowakabili wananchi wa Moshi, zikiwamo za uchumi na siasa.
Ramole ambaye mwaka 2010 aliongoza kura za maoni za ubunge Jimbo la Moshi Mjini, lakini jina lake likakatwa na Kamati Kuu (CC) na kurejeshwa jina la Justine Salakana, alisema atagombea tena kwa kuwa safari hii hakuna mizengwe.
“Nimetangaza nia mapema, baada ya wabaya wangu kuanza kutangaza kuwa sitagombea. Nataka niwahakikishie kuwa nitawania ubunge mwaka 2015,” alisema Ramole.
Mwishoni wa wiki iliyopita, Ndesamburo alisema atatumia kiinua mgongo chake cha ubunge kuhakikisha jimbo hilo linabaki Chadema.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment