KUFUATIA kufungwa kwa ofisi ya aliyekuwa msanii nyota wa filamu marehemu Steven Kanumba ya Kanumba The Great, mama mzazi Flora Mtegoa amegeuka mbogo baada ya kuulizwa kuhusu hatima ya kikazi ya taasisi hiyo.
Muonekana wa Ofisi ya Kanumba The Great wakati ikiwa inafanya kazi.
Watu wamezidi kunifuatilia mambo yangu, sitaki kabisa nimechoka, hii kampuni haimhusu mtu yeyote, hili ni jambo langu siyo lazima niliweke wazi, kama kampuni imekufa au itaendelea haiwahusu, wanaoamini imekufa waamini hivyo, maana hata Yesu walisema atarudi hadi leo mbona hajarudi? aliuliza kwa hasira mama huyo.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, 'Kanumba The Great', Flora Mtegoa.
Ofisi ya mkali huyo wa filamu za Kibongo, aliyefariki ghafla miaka mitatu iliyopita, ilikuwa eneo la Sinza Mori na ilifungwa wiki mbili zilizopita, baada ya mama huyo kudaiwa kushindwa kumudu kodi mpya ya pango ambayo ilipandishwa.
0 comments:
Post a Comment