2015-02-18

MAMILIONI YA DOLA YAIBIWA KATIKA MABENKI KUPITIA WIZI MTANDAO..........bofya hapa kuona video ya wizi huo

Baada ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita chuo kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee duniani kote.

Nategemewa kuwasilisha mada itakayoangazia jitihada za mataifa makubwa 8 dhidi ya uhalifu mtandao na athari za jitihada hizo kwa mataifa mengine katika mkutano wa mwaka utakaofanyika Nchini Croatia unaounganisha wataalam wa maswala ya usalama mitandao kutoka mataifa kadhaa ambapo patajadiliwa mambo kadhaa ya kiusalama mitandao – Taarifa Zaidi za mkutano zinaweza kupatikana kwa "KUBOFYA HAPA"

Wakati haya yakijiri na mikakati Zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika Zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab.


 
Taarifa inaeleza kwamba genge la wahalifu mtandao limefanikiwa kuiba Mamilioni ya Dola za kimarekani kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30 kati ya mwaka 2014 na 2015.
Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya za wahalifu mtandao wanazotumia kudukua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kuiba pesa.

Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao.

Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.

Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.

Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol.Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.

Kamanda wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.

Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.

genge hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu kinachoandakiwa kwenye kompyuta.

Kutokana na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.

Kwa Tanzania Hali inaweza kubadilika kabisa siku za usoni kwani tayari mipango na mikakati ya dhati ya kukabiliana na uhalifu huu wa kuibia watu pesa zao kupitia ATM inaendelea kwa kasi na hatima ya kupata Muarobaini stahiki unategemewa kutatua hali husika.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...